Ustaarabu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
 
Mstari 1:
'''Ustaarabu''' ni aina ya [[utamaduni]] uliyoendelea.
[[Picha:Egypt.Giza.Sphinx.02.jpg|300px|thumbnail|Ustaarabu wa [[Misri ya Kale]] ulibuni ma[[jengo]] ya [[piramidi]] miaka 5000 iliyopita.]]
Katika [[fani]] ya [[historia]] "ustaarabu" (kwa [[Kiingereza]] ''civilisationcivilization'') ni hali ya [[jamii]] iliyoendelea juu ya kuishi katika [[jumuiya]] ndogo zinazojitegema katika mahitaji yote. Kwenye hali ya ustaarabu watu wanashirikiana katika eneo kubwa zaidi, huwa na namna ya [[serikali]]. [[Shughuli]] zinagawanywa kati ya vikundi, ma[[tabaka]] na [[kazi]] mbalimbali chini ya [[kanuni]] na [[sheria]] zinazosimamiwa na mtawala au [[serikali]].
 
Katika historia ustaarabu kwa maana hii ulitokea penye [[kilimo]] ambako wakulima walianza kutoa sehemu ya ma[[pato]] yao kwa mtawala au serikali fulani. Mapato hayo yalitumiwa kugharamia [[jeshi]] au [[silaha]] kwa kutetea jamii, ma[[fundi]] na [[wasanii]], [[ujenzi]] wa [[hekalu|mahekalu]], [[boma|maboma]], [[mfereji|mifereji]] ya [[umwagiliaji]] ma[[shamba]], [[ghala]] kwa mazao n.k.