Bruno Gutmann : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 5:
 
==== Mafunzo ya umisionari ====
Baada ya kutimiza umri wa miaka 18, Bruno alikubaliwa katika [[seminari]] ya Misioni ya Kilutheri huko Leipzig . Kunzia mwaka 1895 alifuata kozi ya kumpa [[elimu ya sekondari]], elimu ya lugha ya [[Kilatini]] na lugha asilia za [[Biblia]] ([[Kiyunani|Kigiriki]] na [[Kiebrania]]) na mafunzo ya [[theolojia]] ya kiprotestanti. Kwenye seminari aliteuliwa kwenda [[Uhindi]], hivyo alijifunza pia [[Kiingereza]], [[Kisanskrit]] na [[Kitamil|Kitamili]]. Gutmann alisoma pia kozi kadhaa kwenye [[Chuo Kikuu cha Leipzig]] alipojiunga na kozi za [[saikolojia]] ya kijamii na [[historia]]. 1901 alimaliza masomo ya theolojia akabarikiwa kuwa mchungaji akatumwa kwa mwaka mmoja kuhudumia kanisa akatikakatika kijiji kidogo ili apate uzoefu wa kazi hiyo kabla ya kuondoka Ujerumani.
 
Aliporudi Leipzig mwelekeo wake ulibadilishwa; Bruno alikubali kubadilishana nafasi na mwanafunzi mwenzake aliyetakiwa kwenda Kilimanjaro lakini aliogopa afya ya mke wake ingekuwa hatarini kwenye mazingira magumu. Gutmann hivyo alipewa wiki chache kusoma misingi ya [[Kiswahili]].
 
==== Hatua za kwanza katika Afrika ====