Ujenzi wa taifa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Rescuing 1 sources and tagging 0 as dead.) #IABot (v2.0.8
 
Mstari 1:
'''Ujenzi wa taifa''' ni mchakato wa kujenga au kuunda [[utambulisho]] wa kitaifa kwa kutumia nguvu ya [[serikali]]. Utaratibu huu unalenga kuunganisha wananchi katika [[taifa]] ili ibakie imara kisiasa katika kipindi kirefu. Ujenzi wa taifa unaweza kuhusisha matumizi ya propaganda au [[maendeleo]] makubwa ya [[miundomsingi]] ili kuendeleza [[Tabaka|matabaka]] ya kijamii na [[ukuaji wa uchumi]].
Hapo awali, ujenzi wa taifa ulifahamika kama juhudi za mataifa mapya huru kujitegemea, hasa mataifa ya [[Afrika]] yaliyoundwa na [[wakoloni]] bila kufikiria mipaka ya [[Kabila|kikabila]] wala mambo mengine.<ref>{{Cite [web |url=http://www.fiuc.org/iaup/esap/publications/umu/detecgrowth.php |title=^ Economic Development &amp; Nation-building in Africa: In Search of A New Paradigm] |accessdate=2018-09-03 |archivedate=2011-09-30 |archiveurl=https://web.archive.org/web/20110930181318/http://www.fiuc.org/iaup/esap/publications/umu/detecgrowth.php }}</ref> <ref> Nation-Building, Propaganda, and Literature in Francophone Africa</ref>
Ujenzi wa taifa ulijumuisha uumbaji wa parafanalia ya juu ya taifa kama vile [[bendera]], [[Wimbo wa Taifa|nyimbo za taifa]], [[sikukuu za kitaifa]], viwanja vya kitaifa, mashirika ya ndege ya kitaifa, [[lugha za taifa]] na [[hadithi]] za kitaifa. Katika ngazi ya ndani, utambulisho wa kitaifa ulihitajika kujengwa kwa kusudi la kuunganisha makundi mbalimbali kuwa taifa, hasa [[ukoloni]] ulipokuwa ukitumia mbinu za kugawanya na kutawala ili kudumisha utawala wake.