Jinai : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Created by translating the page "Crime"
(Hakuna tofauti)

Pitio la 22:26, 21 Februari 2021

Jinai ni kitendo kinachofanywa na mtu ambacho ni kinyume na sheria za nchi au eneo. Kwa hiyo jinai inafafanuliwa na sheria inayotaja matendo maalum kuwa vile.

Matendo yanayotajwa kama jinai hutazamiwa kuwa hatari ya amani katika jamii na pia kuvunja haki za watu. Kwa hiyo katika mifumo ya sheria ya kisasa dola linalenga kulinda amani na haki kwa kutunga sheria zinazokataza jinai. Jinai kwa jumla hutawaliwa na sheria ya jinai, ambayo ni tofauti na sheria ya

Kwa kawaida tendo fulani linahitaji kutendwa pamoja na nia ya kuvunja sheria ili kutajwa jinai. Hata hivyo, pia matendo maalum yanayotendwa "kwa namna ya kutokuwa mwangalifu au kupuuza kwa kiasi cha kuhatarisha maisha ya binadamu au kusababisha dhara kwa mtu mwingine yeyote"[1] yanaweza kuangaliwa kama jinai.

Ilhali kila jinai inavunja sheria, siyo kila unvunjaji wa sheria inayohesabiwa kama jinai. Kuvunja sheria za biashara na mikataba baina ya watu inaweza kufuatiliwa kwa kesi za madai mbele ya mahakama, lakini mara nyingi hazifuatiliwi mara moja na vyombo vya dola.


Marejeo

  1. Kanuni ya Adhabu Tanzania (Penal Code , Chapter 16 of the Laws (revised), Jinai kwa kutojali na kupuuza, ss. 233. ([https://sheriakwakiswahili.blogspot.com/p/downloads.html online hapa])