Tofauti kati ya marekesbisho "Jinai"

371 bytes added ,  miezi 7 iliyopita
no edit summary
Tag: 2017 source edit
Tag: 2017 source edit
'''Jinai''' ni kitendo kinachofanywa na [[Binadamu|mtu]] ambacho ni kinyume na [[sheria]] za [[nchi]] au eneo. Kwa hiyo jinai inafafanuliwa na [[sheria]] inayotaja matendo maalum kuwa vile<ref>[https://sheriakiganjani.co.tz/page.php?key=226<nowiki> Nini maana ya jinai?], tovuti ya Sheria Kiganjani, inayotolewa na Tanganyika Law Society</nowiki></ref>.
 
Matendo yanayotajwa kama jinai hutazamiwa kuwa hatari ya amani katika jamii na pia kuvunja haki za watu. Kwa hiyo katika mifumo ya sheria ya kisasa [[dola]] linalenga kulinda amani na haki kwa kutunga sheria zinazokataza jinai. Kwa hiyo si kazi ya mtu aliyepata madhata kufuatilia jinai, bali ni kazi ya dola.<ref>[https://sheriakiganjani.co.tz/uploads/97731-jinai.pdf Wakili Manace Ndoroma: Kosa la jinai, maelezo na ufafanuzi]</ref>
 
Kwa kawaida tendo fulani linahitaji kutendwa pamoja na nia ya kuvunja sheria ili kutajwa jinai. Hata hivyo, pia matendo maalum yanayotendwa "kwa namna ya kutokuwa mwangalifu au kupuuza kwa kiasi cha kuhatarisha maisha ya binadamu au kusababisha dhara kwa mtu mwingine yeyote"<ref>Kanuni ya Adhabu Tanzania (Penal Code , Chapter 16 of the Laws (revised), Jinai kwa kutojali na kupuuza, ss. 233. ([https://sheriakwakiswahili.blogspot.com/p/downloads.html<nowiki> online hapa])</ref> yanaweza kuangaliwa kama jinai.