Lilian Mary Nabulime : Tofauti kati ya masahihisho

Msanii wa kuchonga kutoka Uganda
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'alt=Lilian Mary Nabulime|thumb|Lilian Mary Nabulime '''Lilian Mary Nabulime''' (alizaliwa tarehe 22 December 1963) ni mhadhir...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 12:07, 6 Machi 2021

Lilian Mary Nabulime (alizaliwa tarehe 22 December 1963) ni mhadhiri wa sanaa na mchonga sanamu wa Uganda. Ni mhandisi wa chuo cha uundaji, Sanaa na teknolojia (CEDAT) na amefanya maonyesho ya kazi zake ndani nan je ya nchi yake. [1]

Lilian Mary Nabulime
Lilian Mary Nabulime

Wasifu

Nabulime alizaliwa wilaya ya Kampala nchini Uganda mwaka 1963 na kusoma shule ya msingi ya wasichana Nkoni. Alisoma shule ya Makerere kwa elimu ya sekondari na upili na baadae kupata shahada ya Sanaa kutoka chuo kikuu cha Makerere mwaka 1987. Alipata shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Makerere na shahada ya uzamivu katika chuo kikuu cha Newcastle mwaka 2007.[2]

Kazi yake

Nabulime ni mhadhiri na pia alishawahi kuwa kiongozi wa idara ya viwanda, Sanaa, chuo cha uhandisi, uundaji, na teknolojia (CEDAT) katika chuo kikuu cha makerere. Kazi yake hutumia vitu vya kawaida kama vile sabuni, chujio, nguo, chupa za chuma na sehemu za magari katika kutengeza taswira na ajenda zinazohusu magonjwa, jinsia na mazingira kwa lengo la kuongeza utambuzi na kuikuza Sanaa.[3][4]

Tuzo zake

  • Commonwealth Fellowship Award UK (2012)[5]
  • Robert Sterling Fellowship, Vermont Studio Center, USA (2011)
  • African Stones Talk Sculpture Symposium (AST), Kenya (2011);
  • British Academy International Visiting Fellowship 2009;[6]
  • ROLS UK (2009 and 2008) and; Commonwealth Fellowship Award, UK (1997).

Marejeo