Ulimwengu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 10:
Kwa [[Kiswahili]] cha kila siku mara nyingi hakuna tofauti kati ya ''Dunia'' na ''ulimwengu''. Lakini kama [[lugha]] inataka kujadili habari kwa undani pamoja na [[ujuzi]] wa siku zetu kuna ulazima wa kutofautisha kati ya [[ngazi]] mbalimbali za [[mazingira]] tunamoishi.
 
Kwa maana hiyo Dunia ni hasa [[sayari]] tunapoishi. Zamani [[watu]] waliona Dunia kwa maana hiyo ni sawa na ulimwengu wote. Lakini [[maendeleo]] ya [[sayansi]] yametuonyesha upeo mkubwa zaidi uliopo ng'ambo ya sayari yetu na hata ng'ambo ya [[mfumo wa jua|mfumo wa Jua]] letu na sayari zake. Kwa hiyo [[neno]] "ulimwengu" limekuwa muhimu kwa sababu linalenga kiasili kwa jumla la vitu vyote si kwa sayari yetu hasa.
 
Katika [[Wikipedia ya Kiswahili|Wikipedia hii]] tunatumia neno "ulimwengu" kama [[Kiingereza]] ''[[:en:universe|universe]] au [[:en:cosmos|cosmos]]''. "Dunia" tunatumia kwa maana ya Kiingereza ''[[:en:earth|earth]]''. Wakati mwingine lugha za [[Ulaya]] zinatumia "universe" karibu sawa na "space" au "outer space" zikimaanisha nafasi kubwa ulimwenguni nje ya Dunia yetu. Hali halisi Dunia yetu ni ndogo sana ulimwenguni na kwa hiyo upeo wa "space" ni karibu sawa na upeo wa "universe". Lakini lugha nyingi zinatofautisha kati ya nafasi ile kubwa nje ya Dunia na dhana ya ulimwengu kama jumla ya vyote.
 
Kwa Kiswahili ni afadhali kutofautisha vilevile. Kwa kawaida tunatumia neno "anga" linalomaanisha kiasili kile kinachong'aa yaani mahali pa [[mwanga]] jinsi ilivyo anga juu yetu inayoangazwa na juaJua. Kutokana na maana hiyo ya msingi "anga" linamaanisha yote ambayo ni juu yetu. Hivyo "anga" linataja mara nyingi [[angahewa]] ya Dunia, au yale ya [[buluu]] yanayoonekana juu yetu. Lakini hutumiwa pia kwa nafasi kubwa nje ya angahewa. Hapa tunatumia pia lugha ya "[[anga-nje]]" tukitaka kutofautisha angahewa na ule uwazi mkubwa kati ya nyota na galaksi.
 
== Ulimwengu na sayansi ==