AK-47 : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Created by translating the page "Kalashnikov rifle"
(Hakuna tofauti)

Pitio la 17:15, 14 Aprili 2021

Bunduki ya Kalashnikov (Калашников) au AK-47 ni aina ya bunduki inayofuata muundo uliobuniwa na mvumbuzi Mikhail Kalashnikov kutoka nchini Urusi. Kuna matoleo tofauti ya bunduki hizo.

Hapo awali zilitengenezwa katika Umoja wa Kisovyeti, lakini bunduki hizi na anuwai zao sasa zinatengenezwa katika nchi nyingi.

Kalashnikov ni moja wapo ya bunduki zinazotumiwa sana ulimwenguni; kwa jumla kuna bunduki milioni 72 zinazopatikana ulimwenguni kote katika nchi karibu 100. [1] [2]

Mfano wa bunduki ya shambulio la Kalashnikov 1974 iliyotengenezwa na Izhmash, Urusi (AK-74)

Historia

Uongozi wa Jeshi Jekundu (jeshi la Umoja wa Kisovyeti) ulitambua wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia dhidi Ujerumani kwamba wangehitaji bunduki mpya inayoweza kutumiwa kwa kufyatua risasi moja-moja lakini pia kwa wingi ikihitajika, kwa namna ya bombomu.

Katika mashindano yaliyotangazwa ndani ya jeshi na tasnia ya silaha, Mikhail Kalashnikov alishinda. Modeli yake ilikuwa tayara mwaka 1947 ikaanza kutengenezwa mwaka 1948. Kifupi cha AK-47 kinamaanisha "Avtomat Kalashnikov 1947" (Автомат Калашникова складной образца 1947 года).

Ni bunduki inayotengenezwa kirahisi inafanya kazi pia katika mazingira magumu kama joto au baridi, mvua au ukame. Hivyo imesambaa sana duniani, na uongozi wa Umoja wa Kisovyeti ilitoka vibali kwa nchi nyingi rafiki ya kuinakili na kuitengeneza kwao.

Uzalishaji

Ubunifu rahisi wa bunduki hufanya iwe rahisi kutolewa, na Umoja wa Kisovyeti ulikodisha mipango ya silaha hiyo kwa nchi rafiki, ambapo ingeweza kutengenezwa kienyeji kwa gharama ya chini. [1] Kama matokeo, bunduki za Kalashnikov na anuwai zao zimetengenezwa katika nchi nyingi, na bila leseni. Nchi za utengenezaji kwa mpangilio wa alfabeti ni pamoja na:

Marejeo

 

Vyanzo

  1. 1.0 1.1 Franko, Blake (2017-05-08). "The Gun That Is in Almost 100 Countries: Why the AK-47 Dominates". The National Interest (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-09-26.  Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name ":0" defined multiple times with different content
  2. McCarthy, Niall. "The Cost Of An AK-47 On The Black Market Around The World [Infographic]". Forbes (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-09-26.