Ingenuity (helikopta) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Created by translating the page "Ingenuity (helicopter)"
(Hakuna tofauti)

Pitio la 12:36, 20 Aprili 2021

Kigezo:Infobox individual space vehicleIngenuity (tamka in-ji-nyu-i-ti; Kiingereza, kwa maana ya ubunifu) ni helikopta ndogo isiyo na rubani iliyopelekwa kwenye sayari ya Mirihi (Mars) kwenye mwezi wa Februari 2021. Ilifika pamoja na gari la upelelezi Perseverance kama sehemu ya mradi wa "Mars 2020" wa mamlaka ya anga-nje ya Marekani NASA.

Ingenuity ni helikopta ya majaribio yanayolenga kuonyesha kama chombo cha hewani kinaweza kutumiwa katika upelelezi wa sayari ya Mirihi.

Ingenuity ni kifaa kidogo; vipimo vya bodi yake havizidi sentimita 20, mikono ya rafadha yake (rotor) ina urefu wa mita 1.2 ikisimama juu ya miguu ya sentimita 30. Uzito wake ni gramo 1800 pekee.

Inabeba kamera mbili, moja inayotazama chini yake na moja ya kupiga picha za mazingira. Kuna redio ndogo ya mawasiliano. Haiwezi kuendeshwa kutoka duniani moja kwa moja kwa sababu alama za redio zinahitaji dakika kadhaa baina ya Mirihi na Dunia, hivyo ina kompyuta ndogo ndani yake inayopokea maagizo kutoka duniani na kudhibiti miendo ya helikopta. Kama kila helikopta, inapaa hewani kutokana na mwendo wa rafadha yake, inayofanana na panka kubwa iliyofungwa juu ya bodi yake. Ina rafadha mbili zenye mwendo wa kinyume kati yake. Hizo zinaendeshwa na injini ya umeme inayopata nguvu yake kutoka kwa beteri. Betri zinachajiwa kwa paneli za sola. Hapa kuna changamoto nyingine yaani baridi ya usiku kwenye Mirihi. Halijoto hushuka hadi nyuzi 90 chini ya sifuri wakati wa usiku, hali inayoweza kuchosha betri haraka sana.

Changamoto kubwa ni angahewa nyepesi ya sayari hiyo; kiasi cha hewa kinachopatikana kinalingana na kimo cha kilomita 30 juu ya uso wa ardhi[1] na hadi sasa hakuna helikopta duniani iliyopaa juu ya kilomita 13[2].

Picha kutoka juu zingesaidia kupanga safari za gari la Perseverance[3][4] ; maana hadi sasa magari kwenye Mirihi yameweza kusafiri polepole sana kwa sababu kila baada ya mwendo wa mita kadhaa, dereva aliye duniani anapaswa kusubiri dakika hadi kupokea picha mpya za eneo lililopo mbele, kuziangalia na kuamua kama ni salama gari liendelee, kutuma maagizo yake kwa kompyuta ya gari na kusubiri tena hadi picha zijazo zimefika. Picha kutoka juu zinaonyesha sehemu kubwa ya eneo litakalopitiwa na hivyo gari lingeweza kwenda mbali zaidi bila kusimama.


Tarehe 19 Aprili 2021 Ingenuity iliruka mara ya kwanza kwa sekunde 39, ikapaa mita 3 hewani na kutua tena.[5] [6][7]


Ingenuity inatarajiwa kuruka hadi mara tano katika muda wa siku 30 za kwanza ikifika kwenye kimo cha mita 3–5 juu ya uso wa Mirihi kwa sekunde 90 kila safari. Imepangwa kutembea kwa umbali wa mita 50 na kurudi.

Ikiwa ujanja unafanya kazi kama inavyotarajiwa, NASA inaweza kujenga juu ya muundo wake ili kupanua sehemu ya angani ya ujumbe wa Mars wa baadaye. Mradi huo unaongozwa na MiMi Aung huko JPL. Wachangiaji wengine ni pamoja na AeroVironment, Inc., Kituo cha Utafiti cha Ames cha NASA, na Kituo cha Utafiti cha Langley cha NASA.

Ujanja hubeba kitambaa kutoka kwa bawa la Wright Flyer ya 1903, ndege ya Wright Brothers, ndege ya kwanza inayodhibitiwa ya wanadamu Duniani, na eneo lake la kuondoka na kutua limepewa jina la uwanja wa Wright Brothers.

Picha

Marejeo

 

Viungo vya nje

  1. Chang, Kenneth (23 June 2020). "Mars Is About to Have Its "Wright Brothers Moment" – As part of its next Mars mission, NASA is sending an experimental helicopter to fly through the red planet's thin atmosphere". The New York Times. Archived from the original on 23 June 2020. [https://web.archive.org/web/20200623070602/https://www.nytimes.com/2020/06/23/science/mars-helicopter-nasa.html online hapa]
  2. [https://archive.ph/20150301211934/http://www.fai.org/fai-record-file/?recordId=754 FAI Record ID #754], tovuti ya Fédération Aéronautique Internationale, FAI - The World Air Sports Federation, ya tarehe 30 April 2012, kupitia archive.org
  3. Chang, Kenneth. "Mars Is About to Have Its "Wright Brothers Moment" – As part of its next Mars mission, NASA is sending an experimental helicopter to fly through the red planet's thin atmosphere.", 23 June 2020. 
  4. Leone, Dan. "Elachi Touts Helicopter Scout for Mars Sample-Caching Rover", SpaceNews, 19 November 2015. 
  5. Palca. "Success! NASA's Ingenuity Makes First Powered Flight On Mars", National Public Radio, 19 April 2021. Retrieved on 19 April 2021. 
  6. Hotz. "NASA’s Mars Helicopter Ingenuity Successfully Makes Historic First Flight", Wall Street Journal, 2021-04-19. Retrieved on 2021-04-19. 
  7. AFP Staff Writers (Apr 19, 2021). Ingenuity helicopter successfully flew on Mars: NASA. Mars Daily. ScienceDaily. Iliwekwa mnamo 2021-04-19.