Rena Callist : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Rena Callist Nyamwelo''' (24 Machi 1970) ni jina la kutaja mjasiriamali, msimamizi wa wanamitindo, mratibu wa matamasha mbalimbali hasa muziki...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 14:26, 25 Aprili 2021

Rena Callist Nyamwelo (24 Machi 1970) ni jina la kutaja mjasiriamali, msimamizi wa wanamitindo, mratibu wa matamasha mbalimbali hasa muziki wa kizazi kipya na dansi, na mkereketwa wa burudani kindakindaki kutoka nchini Tanzania. Rena pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Kings & Queens Worldwide Co. Limited, Rena Events Limited, Kibara Mining Limited na Digital AM Limited.

Mwaka wa 1993, alikuwa miongoni mwa Watanzania wa mwanzo kushirikiana na kampuni ya Coca Cola kuandaa shindano la Ulimwende. Vilevile alisimamia onesho kubwa la disko lililofanyika mwaka 1994 kwa minajili ya kuchangia pesa kwa ajili ya hayati DJ Kalikali (Tanzania DJS Festival).

Mwaka wa 1997 aliwaleta tena watu pamoja katika onesho la "Full Blast Music Show" iliyofanyika jijini Dar es Salaam chini ya udhamini wa kampuni ya bia ya Tanzania (TBL).

Wanamuziki kutoka nje ambao aliwahi kusimamia ujio wao kwa Tanzania ni pamoja na Lucky Dube (1997), Yvone Chakachaka.

Viungo vya nje