Gereza : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 2:
'''Gereza''' (pia: '''jela''', kwa [[Kiingereza]]: ''prison, jail'') ni mahali ambako watu wanalazimishwa kukaa wakishikwa kinyume cha matakwa yao.
 
Kwa kawaida hali ya kufungwa ndani ya gereza ni [[adhabu]] iliyotolewa na [[mahakama]] kwa [[mtu]] aliyevunja [[sheria]]. Mara nyingi watu hufungwa ndani pia wakishtakiwa tu kuvunja sheria wakisubiri [[kesi]] zao zisikiwe mahakamani.
 
Katika nchi kadhaa [[serikali]] inatumia gereza kufunga watu wanaopinga [[viongozi]] wa nchi au kukosoa serikali.
 
==Etimolojia==
[[Asili]] ya [[neno]] la [[Kiswahili]] "gereza" ni [[Kireno]] "[[:pt:igreja|igreja]]" inayomaanisha "[[kanisa]]" (la [[Kikristo]]). Maana imebadilika kwa sababu makanisa ya kwanza ya [[Wareno]] katika [[Afrika ya Mashariki]] yalijengwa ndani ya [[Boma|maboma]] yao. Kwa hiyo ilhali "igreja" ya Wareno ilikuwa ndani ya [[jengo]] imara ya [[ngome]] ilitokea kwamba ngome yenyewe ikaitwa hivyo. Hapo neno jipya "gereza" lilikuwa na maana ya "boma, ngome". Baadaye [[ngome]] hizo hazikuwa tena na kazi ya kijeshi kutokana na [[maendeleo]] ya [[teknolojia]] ya [[silaha]], hivyo zilitumiwa kama jela kutunza wafungwa. <ref>"Etymologically speaking, the Kiswahili word gereza (prison) comes from the Portuguese igreja meaning church. This semantic change can be attributed to hostility greeted on the Portuguese by the then Islamised coastal communities forcing them to build their churches within the precincts of the fortresses." Adika Stanley Kevogo & Alex Umbima Kevogo: Swahili Military Terminology: A Case of an Evolving NonInstitutionalized Language Standard, Research on Humanities and Social Sciences ISSN (Paper) 2224-5766, ISSN (Online) 2225-0484 Vol.4, No.21, 2014, imeangaliwa kupitia https://www.researchgate.net/publication/325157378</ref>
 
Neno "jela" limekopwa kutoka Kiingereza "jail" wakati wa [[ukoloni]] wa Kiingereza.