Stadi za maisha : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '=Stadi za maisha= Maisha ni muambatano wa muda pamoja na matukio,hivyo ni muhimu kufahamu kuwa muda unavyozidi kwenda ndipo kiumbe hai kinapata nafasi ya kupita...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 14:32, 30 Mei 2021

Stadi za maisha

Maisha ni muambatano wa muda pamoja na matukio,hivyo ni muhimu kufahamu kuwa muda unavyozidi kwenda ndipo kiumbe hai kinapata nafasi ya kupita katika matukio mbali mbali yaliyo mazuri na mabaya na yote huitaji hekima na maarifa katika kuyapitia hususan yaliyo mabaya. Nikinukuu msemo wa lugha ya kiswahili unaosema kuwa "KUISHI KWINGI NI KUONA MENGI" maana halisi ni kuwa mtu aliyemtangulia mwenzake kiumri anakuwa na uzoefu mkubwa sana kwasababu ya mambo ambayo amekwisha kuyaona ni mengi katika kuishi kwake na kupitia uzoefu huo ndiyo mtu huyo anapata mbinu nyingi za kumwezesha yeye kukabiliana na nyakati zote katika maisha yake. Haina maana ya kwamba mtu mwenye umri mdogo kwasababu ya kuwa na uzoefu mdogo wakimaisha basi anapaswa kukosa busara na hekima za kumwezesha yeye kuishi vizuri. swali:JE MTOTO MDOGO AU KIJANA ANAWEZAJE KUWA NA HEKIMA KAMA ZA MTU MZEE? jibu:NI KUPITIA KUJIFUNZA STADI ZA MAISHA. ambazo ni kama zifuatazo.

  1. STADI BINAFSI.
  2. STADI ZA KIJAMII.
  3. STADI ZA MAAMUZI SAHIHI.

Stadi binafsi

Hizi ni mbinu au kanuni amabazo zinamwezesha mhusika kuwa na uwezo mkubwa wa kujitambua yeye mwenyewe kwanza kiundani zaidi kwa maana ya hisia,uwezo,madhaifu na nafasi yake katika jamii.stadi binafsi ni muhim sana kwa sababu zinamwezesha mhusika huyo kujijengea hali ya kujiamini kutokana na kuitambua thamani yake katika jamii inayomzunguka. ili kuwa bora katika stadi binafsi mhusika anapaswa kuwa na uwezo katika vitu vifuatavyo.

kujitambua,kutambua mahitaji na kuweka malengo katika maisha

Sadi za kijamii

hizi ni stadi ambazo humjenga na kumwezesha mhusika kujua naamna ya kuishi na watu kwa upendo na amani na kujenga ushirikiano ulio bora.vifuatavyo nni vipengele muhim amabvyo vinamthibitisha mtu kuwa stadi za kijamii.

uwezo wa kujenga mahusiano mazuri na watu wanaokuzunguka

uwezo wa kujitawala kifikra na kuhepuka misukumo asi

uwezo wa kutambua na kujihusisha katika kusaidia changamoto za wanajimii

mawasiliano mazuri

stadi za maamuzi sahihi

hizi ni stadi ambazo zinamwezesha mhusika kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi wakati wa changamoto na yanapotokea machaguo mengi.kama ilivyo katika stadi nyingine hii pia ina kanuni amabazo ndio msingi wa kupatikana kwa maamuzi sahihi,nazo ni kama ifuatavyo.

mawazo chanya

ubunifu wa kimawazo

maono ya mbeleni

uwezo wa kufanya maamuzi

vyanzo vya stadi za maisha

watu hujifunza/kuiga stadi za maisha katika sehemu,makundi au watu mbalimbali ila sehemu au vitu amabavyo ndio msingi wa stadi za maisha ni hizi zifuatazo.

Familia zetu.

hapa tunajifunza na kuiga vitu kutoka kwa wazazi au ndugu zetu kwasababu tunaishi nao kwa muda mreefu hususani katika kipindi cha ukuaji wetu ambacho ndio kipindi vichwa vyetu vinadaka na kukariri mambo mengi.

Taasisi za kielimu.

hapa mara nyingi ni kupitia maarifa tunayopata kwa kufundishwa na wakufunzi hususadi mashuleni, vyuoni na kadhalika.

Jamii zetu.

tofauti na familia kuna kundi jingine kubwa ambalo linatuzunguka hivyo na lenyewe pia linamchango katika kutujenga kifikra na kuenedeleza stadi zetu za kimaisha.

Imani/Dini.

imani tofauti tofauti zimekuwa zikitoa mafunzo mengi ya kidini amabayo yamekuwa yakihusika katika kuwajenga wahumini wake.kwamfano imani ya kikristo imekuwa ikifundisha juu ya amri kuu ya upendo kitu ambacho ni stadi muhimu inayowezesha mtu kuishi vizuri na watu katika jamii yake.

imeandaliwa na BRIAN PATRICK MANI:ALFAGEMS SECONDARY SCHOOL