Dumuzi mkubwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa mpya
(Hakuna tofauti)

Pitio la 20:31, 22 Julai 2021

Dumuzi mkubwa
(Prostephanus truncatus)
Dumuzi mkubwa juu ya punje za mahindi
Dumuzi mkubwa juu ya punje za mahindi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Coleoptera (Wadudu wenye mabawa magumu)
Nusuoda: Polyphaga
Familia ya juu: Bostrichoidea
Familia: Bostrichidae
Nusufamilia: Dinoderinae
Jenasi: Prostephanus
Lesne, 1898
Spishi: P. truncatus
Horn, 1878

Dumuzi mkubwa (pia scania au Osama (Kenya); kisayansi Prostephanus truncatus) ni spishi ndogo ya mbawakawa ya familia Bostrichidae katika oda Coleoptera ambaye ni msumbufu wa hatari kwa sababu anaharibu nafaka zinazohifadhiwa maghalani. Spishi nyingine ya familia hii ni dumuzi mdogo (Rhyzopertha dominica) ambaye ni 67% ya saizi ya dumuzi mkubwa, lakini ni msumbufu mbaya vilevile.

Maelezo

Dumuzi mkubwa ina urefu wa mm 3-4.5 kulinganisha na urefu wa mm 2-3 mm katika dumuzi mdogo. Mpevu ana umbo la mcheduara la kawaida la Bostrichidae na ncha ya nyuma inayoonekana kama imekatwa. Kichwa kimefichwa kutoka juu chini ya pronoto. Uso wa mwili una vijishimo na chembe nyingi ndogo ndogo kama sugu (vinundu). Vipapasio vina pingili 10 na vina kirungu chenye pingili tatu, ambazo ile ya mwisho ni pana sawa au zaidi kuliko pingili zilizotangulia. 'Shina' la kipapasio ni jembamba na limefunikwa kwa nywele ndefu[1][2].

Mabuu ni weupe na wororo na wamefunikwa kwa nywele habahaba. Pande zao ni sambamba, yaani hazipunguzi. Miguu ni mifupi na kidonge cha kichwa ni kidogo kulinganisha na saizi ya mwili.

Katika hali nzuri ya unyevuanga wa 80%, 32°C na chakula kinachopatikana, dumuzi mkubwa anakamilisha mzunguko wa maisha ndani ya siku 27. Ni msumbufu wa hatari wa nafaka zilizokauka, haswa mahindi, na mahogo yaliyokauka katika sehemu nyingi za Afrika na mabara mengine.

Msambao

Dumuzi mkubwa ni wa asili katika sehemu za tropiki za Amerika ya Kusini, Amerika ya Kati na kusini kabisa mwa Marekani kama msumbufu muhimi, lakini kwa mahali, wa mahindi yaliyohifadhiwa shambani. Aliwasilishwa nchini Tanzania, labda mwishoni mwa miaka ya 1970, na amekuwa msumbufu mbaya wa mahindi na mahogo yaliyohifadhiwa katika sehemu hiyo ya Afrika ya Mashariki. Tangu hapo amesambaa hadi Kenya, Burundi, Rwanda, Malawi, Zambia, Msumbiji, Namibia na Afrika Kusini, na hakika yumo katika nchi nyingine kadhaa za eneo hilo lakini hajaripotiwa. Alipatikana huko Afrika ya Magharibi kwanza katika Togo mnamo 1984, ambapo labda aliwasilishwa kupitia uingizaji wa nafaka kutoka Amerika ya Kaskazini. Tangu hapo amesambaa mpaka Benin, Nijeria, Ghana, Nijeri na Burkina Faso. Mlipuko tofauti ulitokea Gini.

Dumuzi mkubwa anaweza kuvamia maeneo yote ya Afrika ya kitropiki na ya kinusutropiki ambapo muhindi na muhogo inakuzwa, na ni mfano wa pekee wa hivi karibuni wa msumbufu mbaya wa mavuno yanayohifadhiwa anayevamia kwa kiwango cha kikanda au bara zima. Anabaki kuwa tishio la karantini kwa maeneo mengine katika Dunia ya Kale ambapo muhindi unakuzwa.

Mwenendo

Dumuzi mkubwa ni msumbufu wa hatari wa mahindi na viazi vikavu vya muhogo zinazohifadhiwa, na atashambulia mahindi shambani kabla ya uvuno. Majaribio ja kukuza spishi hiyo kwenye kunde, maharagwe, kakao, buni na mchele usiokobolewa katika maabara hayakufanikiwa, ingawa ukuaji unawezekana kwenye aina nyororo za ngano na ulaji wa wapevu unaweza kuharibu bidhaa hizi nyingine.

Dumuzi mkubwa hutenda kama msumbufu wa kawaida wa mahindi yaliyohifadhiwa shambani. Punje nzima hushambuliwa kwenye mabunzi kabla na baada ya kuvuna. Pia ni msumbufu wa mahogo yaliyohifadhiwa shambani, haswa chipsi za muhogo. Wapevu hutoboa vyakula vingi na vitu vingine vikiwemo kuni, mwanzi, plastiki na sabuni. Idadi kubwa za dumuzi wakubwa hutokea katika mazingira ya asilia na wamerekodiwa juu ya spishi kadhaa za miti huko Amerika ya Kati (Rees et al., 1990; Ramirez-Martinez et al., 1994) na Afrika (Nang'ayo et al., 1993, 2002; Nansen et al., 2004) katika visa vingine wakioanishwa na mbawakawa vipapasio-virefu wanaotoa miviringo ya gome kutoka vitawi (Borgemeister et al., 1998).

Uvamizi wa mahindi unaweza kuanza kwenye mazao yaliyokomaa shambani, k.m. wakati unyevu umekuwa sawa na au chini ya 18%. Kupunguza uzito hadi 40% kumerekodiwa katika mabunzi yaliyohifadhiwa kwa muda wa miezi 6 (Giles na Leon, 1975). Nchini Tanzania madhara ya hadi 34% yameonekana baada ya kuhifadhi mahindi kwa muda wa miezi 3 shambani, na dhara la wastani ni 8.7% (Hodges et al., 1983). Dumuzi mkubwa ni msumbufu anayeharibu zaidi kuliko wadudu wengine wa kuhifadhi, pamoja na kidungadunga wa mchele (Sitophilus oryzae), kidungadunga wa mahindi (S. zeamais) na nondo wa nafaka (Sitotroga cerealella), katika hali sawa. Madhara yanayosababishwa na dumuzi mkubwa kwenye viazi vikavu vya muhogo yanaweza kuwa makubwa sana. Wapevu wanaotoboa viazi hivyo huvipunguza kwa urahisi kuwa vumbi na dhara la 70% limerekodiwa baada ya miezi 4 tu ya kuhifadhi shambani (Hodges et al., 1985). Dumuzi mkubwa yuko Afrika ya Magharibi, ya Mashariki na ya Kusini.

Picha

Marejeo

  1. [1] Dumuzi kwenye EAFRINET
  2. [2] Dumuzi kwenye CABI