Dumuzi mkubwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Nyongeza marejeo
Nyongeza matini kuhusu udhibiti
Mstari 40:
 
[[Uvamizi]] wa mahindi unaweza kuanza kwenye mazao yaliyokomaa shambani, k.m. wakati [[unyevu]] umekuwa sawa na au chini ya 18%. Kupunguza uzito hadi 40% kumerekodiwa katika mabunzi yaliyohifadhiwa kwa muda wa [[mwezi|miezi]] 6<ref>Giles, P.H. & Leon, O. (1975) Infestation problems in farm-stored maize in Nicaragua. In: ''Proceedings of the 1st International Working Conference on Stored Products Entomology'', Savannah, Georgia, USA, 1974: 68-76.</ref>. [[Nchi]]ni [[Tanzania]] madhara ya hadi 34% yameonekana baada ya kuhifadhi mahindi kwa muda wa miezi 3 shambani, na dhara la wastani ni 8.7%<ref>Hodges, R.J., Dunstan, W.R., Magazini, I. & Golob, P. (1983) An outbreak of ''Prostephanus truncatus'' (Horn) (Coleoptera: Bostrichidae) in East Africa. ''Protection Ecology'', 5(2): 183-194.</ref>. Dumuzi mkubwa ni msumbufu anayeharibu zaidi kuliko wadudu wengine wa kuhifadhi, pamoja na [[kidungadunga wa mchele]] (''Sitophilus oryzae''), [[kidungadunga wa mahindi]] (''S. zeamais'') na [[nondo wa nafaka]] (''Sitotroga cerealella''), katika hali sawa. Madhara yanayosababishwa na dumuzi mkubwa kwenye [[kiazi|viazi]] vikavu vya muhogo yanaweza kuwa makubwa sana. Wapevu wanaotoboa viazi hivyo huvipunguza kwa urahisi kuwa [[vumbi]] na dhara la 70% limerekodiwa baada ya miezi 4 tu ya kuhifadhi shambani<ref>Hodges, R.J., Meik, J. & Denton, H. (1985) Infestation of dried cassava (''Manihot esculenta'' Crantz) by ''Prostephanus truncatus'' (Horn) (Coleoptera: Bostrichidae). ''Journal of Stored Products Research'', 21(2):73-77.</ref>. Dumuzi mkubwa yuko [[Afrika ya Magharibi]], ya Mashariki na [[Afrika ya Kusini|ya Kusini]].
 
==Udhibiti<ref name="CABI" />==
===Kugundua na kufuatilia===
Kabla ya kuanzisha hatua za [[udhibiti wa wadudu wasumbufu|kudhibiti]] dumuzi mkubwa, ni muhimu kwanza kujua ikiwa msumbufu huyo yupo katika eneo. Hii inaweza kufanywa kwa kutumia [[mtego|mitego]] ambayo ina [[feromoni]] ya madume ya kukusanyika. Mitego hii inapaswa kuwekwa angalau [[m]] 100 kutoka kwenye mashamba ya mahindi au maghala yaliyo na mahindi au mahogo yaliyokaushwa ili kuepusha kuvutia mbawakawa kwenye chanzo cha chakula chao<ref>Hodges, R.J. & Pike, V. (1995) How to use pheromone traps to monitor the Larger Grain Borer (''Prostephanus truncatus''). Chatham Maritime, Kent, UK: Natural Resources Institute.</ref>. Kwa ufuatiliaji wa muda mrefu, mitego iliyotengenezwa kwa [[mbawakawa wa Japani]] ("Popillia japonica") na iliyo na feromoni ya dumuzi mkubwa hutumiwa siku hizi kwa mafanikio katika Afrika ya Magharibi na ya Mashariki.
 
===Aina sugu na usafi===
Mbinu bora ya kudhibiti itakuwa matumizi ya aina sugu za mahindi, ingawa nyingi bado hazijapatikana na kazi nyingi bado inahitajika kufanywa.
 
Ni muhimu sana kutumia maghala yaliyo rahisi kusafishwa. Ni wazi kwamba hatua zozote za maisha za dumuzi mkubwa zitaanza vamizi mpya.
 
===[[Dawa ya kikemikali|Dawa za kikemikali]]===
Dawa za aina ya [[pareto]], kama [[permethrin]] na [[deltamethrin]], hufanya kazi vizuri dhidi ya dumuzi mkubwa lakini hazina ufanisi sana dhidi ya wasumbufu wengine wa uhifadhi. Kwa hivyo, dawa hizi mara nyingi huchanganywa na vifundiro vya [[organofosfati]], kama [[pirimiphos]] na [[fenitrothion]]<ref>Golob, P. & Hanks, C. (1990) Protection of farm stored maize against infestation by ''Prostephanus truncatus'' (Horn) and ''Sitophilus'' species in Tanzania. ''Journal of Stored Products Research'' 26(4): 187-198.</ref>. Maghala makubwa yanaweza kufukizwa kwa [[fosfini]].
 
===[[Udhibiti wa kibiolojia]]===
Mbawakawa [[mbuai]] ''[[Teretrius nigrescens]]'' ametolewa Afrika ya Magharibi na ya Mashariki<ref>Borgemeister, C., Holst, N. & Hodges, R.J. (2003) Biological control and other pest management options for larger grain borer ''Prostephanus truncatus''. In: Neuenschwander, P., Boregemeister, C. & Langewald, J. (eds.) ''Biological Control in IPM Systems in Africa.'' Wallingford, UK: CABI Publishing, 311-328.</ref>. Ingawa kwa kweli amepunguza idadi ya dumuzi mkubwa, akiwa mbuai hafanyi kazi vizuri kama vile [[kidusia|vidusia]]<ref>Holst, N., Meikle, W.G. & Markham, R.H. (2000) Grain injury models for ''Prostephanus truncatus'' (Coleoptera: Bostrichidae) and ''Sitophilus zeamais'' (Coleoptera: Curculionidae) in rural maize stores in West Africa. ''Journal of Economic Entomology'' 93(4): 1338-1346.</ref>. Kwa hivyo, milipuko ya dumuzi mkubwa bado hufanyika mara kwa mara inayohitaji hatua za udhibiti. ''T. nigrescens'' hakujilowea kwa urahisi nchini Tanzania kwa sababu isiyojulikana.
 
Jitihada zimefanywa kudhibiti dumuzi mkubwa katika maghala kwa [[kuvu]] ''[[Beauveria bassiana]]''. Walakini, kuvu haziwezi kufikia mabuu ndani ya punje na wapevu huweza kutaga mayai kabla ya kuuawa na kuvu.
 
==Picha==