Zaghouan : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Zaghwan''' (au '''Zaghouan'''; Kiarabu زغوان ''{{audio|Za8ouen.wav|Zaġwān|help=no}}'') ni mji katika kaskazini ya Tunisia uliopo takriban kilomita 100 upande wa mji mkuu Tunis na km 50 kutoka mwambao wa Bahari ya Mediteranea. Ni makao makuu ya Wilaya ya Zaghouan. Iko juu ya milima midogo ya Dorsale; kutokana na kimo chake hakina joto kali na hali ya maji ni nzuri. Zamani kulikuwa na mifereji ya juu iliyopeleka maji hadi Karthago....'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 14:48, 31 Julai 2021

Zaghwan (au Zaghouan; Kiarabu زغوان  Zaġwān ?) ni mji katika kaskazini ya Tunisia uliopo takriban kilomita 100 upande wa mji mkuu Tunis na km 50 kutoka mwambao wa Bahari ya Mediteranea. Ni makao makuu ya Wilaya ya Zaghouan.

Iko juu ya milima midogo ya Dorsale; kutokana na kimo chake hakina joto kali na hali ya maji ni nzuri. Zamani kulikuwa na mifereji ya juu iliyopeleka maji hadi Karthago.

Mji ni maarufu kwa mashaba yake ya maua ya waridi; kilimo hicho kilianzishwa na wakimbizi Waislamu kutoka Hispania katika karne ya 17.

Upande wa kusini mwa mji kuna magofu ya hekalu ya maji ya enzi za Kiroma iliyokuwa mwanzo wa mfereji wa juu wa maji kwenda Karthago.

Picha

References