Kanada ya Juu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '350px|thumb|Maeneo ya kanada ya Juu katika Kanada ya leo '''Kanada ya Juu''' ''(Kiing. Province of Upper Canada. Kifar. Province du Haut-Canada)'' ilikuwa jimbo la kihistoria katika Amerika ya Kaskazini ya Kiingereza (leo Kanada). Jimbo hili lilianzishwa mnamo 1791 na Uingereza kutokana na maneneo yaliyowahi kuwa sehemu za Jimbo la Quebec. Jina lilichaguliwa kutokana na mwendo wa Mto Saint Lawrence maana...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 23:16, 3 Agosti 2021

Kanada ya Juu (Kiing. Province of Upper Canada. Kifar. Province du Haut-Canada) ilikuwa jimbo la kihistoria katika Amerika ya Kaskazini ya Kiingereza (leo Kanada).

Maeneo ya kanada ya Juu katika Kanada ya leo

Jimbo hili lilianzishwa mnamo 1791 na Uingereza kutokana na maneneo yaliyowahi kuwa sehemu za Jimbo la Quebec. Jina lilichaguliwa kutokana na mwendo wa Mto Saint Lawrence maana lilikuwa na sehemu za juu za beseni ya mto ilhali Quebec yenyewe ilikuwa na sehmu za chini za beseni hiyo.

Kanada ya Juu ilikuwa kimbilio cha watu kutoka sehemu zilizoendelea kuwa Marekani, wakiamua kumfuata mflme wa uingereza na kutoshikamana na uasi wa watu wa majimbo ya Marekani dhidi ya mfalme.

Leo hii sehemu za Kanada ya Juu ya awali zimekuwa sehemu za Jimbo la Ontario katika Kanada. Sheria na siasa za Kanada ya Juu zilifuata kwa karibu mfano wa Uingereza.