Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 50:
==Tafsiri na Jamii==
Salamu, katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Roy_Mugerwa ,Kiswahili kilichotumika kina dalili ya kutungwa kwa kutumia tafsiri ya kompyuta na hivyo kufanya makala kuwa haieleweki, ni vyema kuiboresha zaidi na kuipitia kwanza kabla ya kuendelea na makala nyingine, pia ni vyema kuweka jamii ambazo tayari zipo kuliko kuweka jamii nyingi katika makala na wakati jamii hizo zote hazipo na nyingine hazina mahusiano kabisa na makala, Amani sana '''[[Mtumiaji:Idd ninga|Idd ninga]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Idd ninga|majadiliano]])'''
::Ndugu Godson,umeambiwa kitambo kwamba makala hiyo ina kasoro kwa sababu ulitumia programu ya kutafsiri bila kusoma makini ulichopata lakini hujasahihisha wala kujibu. Umeambiwa huko juu kwamba ni marufuku kumwaga matini kutoka programu hizo hapa kwa sababu kwa njia hii unaleta lugha isiyoeleweka na kusababisha kazi nyingi kwa wengine wanaojitahidi kusafisha kasoro zako. Mfano: "Kazi ya Dkt Mugerwa ingeondoa zuio la moyo baada ya ugunduzi wa VVU / UKIMWI kuwapo nchini Uganda" - sasa je "zuio la moyo" ni kitu gani??? (umekosa maana ya sentensi ya Kiingereza kabisa!) - tena hujajibu hapa ambayo si tabia nzuri. Ilhali naangalia sasa hivi makala nyingine uliyoleta([[Tom von Prince|hiyo!]]), tena bila kuangalia vema ulichomwaga, ninakuonya sasa. Ninakuzuia leo kwa siku moja tu. Unaweza kujibu hapa lakini huwezi kuhariri kurasa nyingine. Unaombwa kueleza jinsi unavyotakla kuendelea. Naona huna nia mbaya, pia unaleta makala za maana lakini hatuwezi kukubali mtindo wa kumwaga google translate bila kujali matokeo. Naombe ujieleze! '''[[Mtumiaji:Kipala|Kipala]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Kipala|majadiliano]])''' 10:13, 7 Agosti 2021 (UTC)