Paul Bomani : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
ANZISHA MAKALA MPYA
(Hakuna tofauti)

Pitio la 17:53, 18 Agosti 2021

Paul Lazaro Bomani alizaliwa tarehe 1 Januari mwaka 1925 na alifariki tarehe 1 Aprili mwaka 2005 alikuwa mwanasiasa wa Tanzania na balozi wa Marekani na Mexico.

Paul Bomani


Kazi

Mnamo mwaka 1960, Bomani alikua Waziri wa Maliasili na Maendeleo ya Ushirika katika serikali ya Tanganyika (1961-1964). Alishikilia nyadhifa zingine kadhaa za uwaziri. Kati ya mwaka 1972 na mwaka1983 alikuwa balozi wa Marekani na Mexico. Kuanzia mwaka 1992 hadi umauti ulipomkuta alikuwa mwenyekiti wa Tanzania Breweries Limited na Tanzania Distilleries Limited,kuanzia mwaka 1993 alikuwa kansela wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.[1]

Bomani alipenda kujielezea kwa maneno yake mwenyewe hivi:Profesa wa Chuo alinielezea kama mbunifu mwenye busara, na kipawa cha kupanga na kuhamasisha watu. Nilikuwa mkono wa kulia wa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa kupigania uhuru. Wasukuma walikuwa kabila kubwa zaidi nchini Tanganyika na walikua zaidi ya robo ya wakazi wa nchi hiyo wanaoishi katika ukanda wa Ziwa. Niliweza kusaidia machifu 50 wa jadi ya kisukuma na kuwapa uaminifu na heshia kubwa. Kwa sababu ya mafanikio ya mashirika yetu ya kijamii na biashara ambayo ilikuwepo kabla ya kuundwa kwa TANU pia niliweza kupata heshima na imani kubwa kutoka kwa watu wa kisukuma , ambao walinipa jina la utani la "Kishamapanda" - maana yake ni "mtengeneza njia".Alifanya kazi zifuatazo:- 1961 Waziri wa Maliasili na Maendeleo ya Ushirika.

1962 Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Tanganyika

1964 Waziri wa Fedha na Masuala ya Uchumi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

1965 Waziri wa Mambo ya uchumi na Mipango ya maendeleo

1970 Waziri wa Biashara, Viwanda na Madini

1972 -1983 Balozi wa Merika ya Amerika na Jamhuri ya Mexico

1983 Waziri wa Rasilimali Madini na Madini

1984 Waziri wa Ardhi, Maliasili, Utalii na Nyumba

1986 Waziri wa Kilimo na Masoko

1988 Waziri wa Kazi na Ustawi wa Jamii

1989 Waziri wa Serikali za Mitaa, Masoko, Ushirika na Maendeleo ya Jamii

1990 Ofisi ya Waziri wa Rais, inayohusika na Utekelezaji na Uratibu Sera ya Baraza la Mawaziri


Viunga vya nje

BOMANI, Paul Lazaro, MA, Tanzanian diplomat, politician; born January 1, 1925, Musoma, Tanzania; married, Kessi Hildegard, six daughters, three sons; education: Ikizu Secondary School, Loughborough College, England, 1953–54, Johns Hopkins University Kigezo:Tanzanian Finance Ministers

Marejeo

  1. Late Ambassador Paul Bomani's Curriculum Vitae. Official Website. Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-09-28. Iliwekwa mnamo 2007-08-02.