Mabantu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
draft
(Hakuna tofauti)

Pitio la 19:13, 28 Septemba 2021

"Mabantu" ni jina la kutaja kundi la muziki wa Bongo Flava kutoka jijini Dar es Salaam, Tanzania. Kundi linaundwa na wasanii wawili, Twarha Kanengo (Twarha Mabantu-9 Julai, 1997) na Mwarami Kajonje (Mwarami Mabantu-21 Januari, 1999).

Mabantu
Kazi yakeWanamuziki
Miaka ya kazi2018
Ameshirikiana naWhozu, Young Lunya

Kwa pamoja, wanafahamika kwa wimbo wao Sundi (2018), Bodaboda (2018) "Kama Tulivyo" (2019) wakimshirikisha Whozu, na ule maarufu zaidi ni Nawakera walishirikiana na Young Lunya. Pia waliwahi kufanya kazi ya kishirikishi na R "the" DJ, Shobo (2021).

Mabantu walikuja kutambulika zaidi kupita kiasi baada ya kutoa Sponsa (2020), walirudi tena na Young Lunya.

Historia

Hapo awali, wawili hawa wote walikuwa katika taasisi ya Said Fella, maarufu kama "Mkubwa na Wanawe" wakiwa sehemu ya wasanii wanaosubiri kuwezeshwa. Ilipotimu mnamo mwaka wa 2013, kabla hata ya kushiriki katika wimbo hata mmoja, vijana hawa waliamua kuondoka mikononi mwa mkubwa na wanawe, na hatimaye kuanzisha Mabantu rasmi.

Mwarami aliingia Mkubwa na Wanawe mwishoni mwa 2011, wakati Twarha aliingia 2012 mwishoni. Lakini lilipokuja suala la kutaka kujiendeleza zaidi nje ya mikono ya kituo cha Mkubwa Fella, iliwalazimu waje na jina la kundi ambalo wangelitumia kama utambulisho kwa wasanii hawa.

Wakiwa kituoni kwa Fella, walipata fursa ya kushiriki mazoezi mbalimbali ya kuondoa uwoga wa hadhira na matumizi ya ala za sauti na vyombo vya muziki. Kituo kilikuwa na kila aina ya vifaa wezeshi kwa watoto wanaokaa hapo. Walirekodi nyimbo kadhaa ambazo hazikutoka nje ya kituo hicho. Kimsingi, Twarha ni mnenguaji na mwimbaji, wakati Mwarami alijipambanua kama mwimbaji zaidi.

Nyimbo maarufu

Marejeo