Kampeni za Kivita katika Afrika ya Mashariki (Vita ya Kwanza ya Dunia) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Rescuing 1 sources and tagging 0 as dead.) #IABot (v2.0.8
Mstari 42:
Katika Msumbiji aliweza kuteka kambi ya kijeshi ya Wareno alipokamata bunduki na risasi pamoja na chakula. Waingereza walijaribu kumfuata laini walishindwa kumkuta katika Msumbiji. Katika miezi ya 1918 iliyofuata Lettow Vorbeck alizunguka katika Msumbiji ya kaskazini, mara nyingi kwa umbali wa matembezi ya siku 2 au tatu na Waingereza na Wareno waliomtafuta bila kumpata. Alivamia vituo mbalimbali vya Wareno na kupata risasi na vyakula mara kwa mara.
[[Picha:Lettow's surrender.jpg|thumb|250px|Jeshi la Kijerumani ilivyosalimisha amri 1918 (uchoraji wa siku zile)]]
Katika Septemba 1918 alipata habari ya kwamba Waingereza walikuwa nyuma yake kwa jeshi kubwa. Hapa aliamua kurudi Tanganyika na kuelekea [[Rhodesia]] kwa sababu habari zilimfikia ya kwamba Waingereza hawakuwa tena na jeshi huko. Tarehe 28 Septemba alivuka tena [[mto Rovuma]] akaendelea katika sehemu za kusini kupitia Songea na Mbozi. Mwezi wa Novemba aliingia Rhodesia ya Kaskazini ([[Zambia]]). Tarehe 13 Novemba kikosi chake kiliteka mji wa [[Kasama]] ambako Waingereza wachache walikimbia walipomwona. Siku iliyofuata afisa Mwingereza alikaribia kambi yake na kumletea habari ya kwamba vita ilikwisha tayari na Ujerumani iliwahi kusimamisha mapigano yote tangu 11 Novemba 1918. Lettow alipatana na Waingereza kuongoza askari hadi mji wa Abercorn (leo [[Mbala, Zambia]]) aliposalimisha amri tarehe 23 Novemba 1918.
 
Askari na maafisa wa Schutztruppe waliongozwa na Waingereza kutoka hapa hadi [[Bismarckburg]] ([[Kasanga (Ufipa)|Kasanga]]) walipowekwa kwenye meli hadi Kigoma. Kutoka hapa walisafirishwa kwa [[reli ya kati]] hadi Tabora ambako askari Waafrika wa Schutztruppe waliweza kurudi makwao. Wajerumani waliendelea hadi Dar es Salaam. Baada kusubiri wiki kadhaa waliondoka kwenye Januari 1919 kwa meli hadi Ujerumani.<ref>Schnee, Heinrich: Deutsch-Ostafrika im Weltkriege, Leipzig, 1919, uk. 406</ref>
 
==Tanbihi==