Hassan bin Omari : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Removing 'Maji_maji_rebellion'_monument.jpg, it has been deleted from Commons by Yann because: Copyright violation, see c:Commons:Licensing.
Removing Projectiles(bullets)_of_Hassan_bin_Omari_(Makunganya).jpg, it has been deleted from Commons by Regasterios because: No license since 21 Oct
Mstari 29:
==Shambulio dhidi ya Boma la Ujerumani, Kilwa Kivinje, mwaka wa 1894==
Mapema Septemba, ilisikiwa kuwa watu wa Mavuji wameharibu laini ya simu kati ya [[Mohoro]] na Kilwa. Siku chache baadaye, [[alfajiri]] ya tarehe 7 Septemba 1894, kufuatia uvumi mwingi, watu wa Hassan bin Omar, pamoja na Wayao kwa maelfu, walipiga risasi kwenye kituo cha Kilwa, na wakapepea bendera mbili nyekundu za Sultan wa Zanzibar.<ref>Meinecke, Gustav Hermann. Aus dem Lande der Suaheli: Reisebriefe und Zuckeruntersuchungen am Pangani. Germany: Deutscher Kolonial-Verlag, 1895.</ref> [[Msikiti]] wa karibu uliingiwa na mashaka katika matata haya kwa sababu ya sauti kubwa au kelele zilizotokea wakati wa [[sala]] ya 'fajr'. Milio mikali ya risasi iliendelea pande zote mbili, na [[mizinga]] ilipigwa na wao ndani ya kituo. Karibu saa sita za mchana, majirani ya kituo yalikuwa yametulia, na watu wa Hassan bin Omari walikuwa wamerudi nyuma. Kwa upande wa Wajerumani, mzungu mmoja na askari wanne wa rangi walijeruhiwa, na upande wa Wamavuji walifiwa 37, na hawa wakaachwa karibu na kituo hicho. Baada ya mambo haya, wafungwa kadhaa walinyongwa wakati Luteni [[Kanali]] von Trotha alipokuja Kilwa. Zilisikiwa pia habari wakati huu kwamba mikebe 600 ya [[baruti]], makasha 6 ya mirao, na [[sanduku|masanduku]] 10 ya fedha vilipelekwa kwa chombo kutoka Zanzibar kwenda Mtapatapa, kufikishwa mikononi Hassan bin Omari.<ref>Aus Deutsch-Ostafrikas Sturm- und Drangperiode; Becker, Alexander Halle, [1911]</ref>
 
[[File:Projectiles(bullets) of Hassan bin Omari (Makunganya).jpg|thumb|8 risasi za Mavuji (Hassan bin Omari)]]
Katika "Shairi la Makunganya", ingawa ni [[utenzi]] wakusifia Wissmann mno, na bali kushahidi matata haya mwenyewe, mshairi amelitunga kutokana na kisa zilizosikia yeye muda fupi baadaye, inadaiwa kwamba Hassan bin Omari alikuwa na mpango wa kumkamata Wissmann mwenyewe, bila Omari kujua kwamba yeye amekwisha ondoka mjini kwa muda, na dhana ile ile hupatikana pia katika [[magazeti]] ya habari za wakati huu.<ref name="Sache1898" />