Simon Patrick : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Simon Mshubirwa Patrick''' ni Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama wa klabu ya mpira wa miguu maarufu Dar Young Africans kutoka nchini Tanzania. Amekuwa akitumikia cheo hiki tangu 2019. Pia amewahi kushika wadhifa wa Katibu Mkuu wa Yanga mnamo 15 Juni, 2020, ni baada ya Yanga kuachana na Katibu Mkuu wake wa zamani Dk. David Luhago kwa kile kilichodaiwa 'kwa maslahi mapana ya klabu.<ref>{{Cite web|title=YANGA SC YAACHANA NA KATIB...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 05:26, 7 Novemba 2021

Simon Mshubirwa Patrick ni Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama wa klabu ya mpira wa miguu maarufu Dar Young Africans kutoka nchini Tanzania. Amekuwa akitumikia cheo hiki tangu 2019. Pia amewahi kushika wadhifa wa Katibu Mkuu wa Yanga mnamo 15 Juni, 2020, ni baada ya Yanga kuachana na Katibu Mkuu wake wa zamani Dk. David Luhago kwa kile kilichodaiwa 'kwa maslahi mapana ya klabu.[1]'

Novemba 17, 2020, klabu ilimsimamisha Simon katika nyadhifa zake mara moja na kuagiza uchunguzi dhidi yake. Taarifa ilitolewa na Mshindo Msolla. Hata hivyo, tarehe 2 Juni, 2021 walimrudisha kazini na cheo chake cha zamani kama 'Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama wa Yanga.'[2]

Katika tuhumu hizo zilizopelekea kung'olewa mbawa zake za kimamlaka, kamati huru iliyoundwa kuchunguza ilibaini kuwa si kweli kwamba alihusika katika kuhujumu kuondoka kwa Bernard Morrison Yanga. Pia si kweli kwamba alitoa faili la kisheria Yanga na hata kukutana na mmoja wa wanachama hasimu wa klabu ya Yanga Oktoba 20, 2020.[3]

Mnamo tarehe 30 Mei, 2020, Mwenyekiti wa Yanga Msindo Msolla alimfutia tuhuma zote zilizokuwa zinamkabili Simon na kuomba kuungwa kwa Simon na wanachama wa Yanga.[4]

Amekuwa akidumu katika wadhifa huo tangu hapo.

Maisha na elimu

Simon ni wakili msomi aliyepata elimu ya uwakili katika vyuo mbalimbali nchini Tanzania. Mwaka wa 2016, alipata Stashahada ya Uzamili katika masuala ya sheria kutoka katika Chuo cha Sheria cha Dar es Salaam (The Law School of Tanzania, Dar es Salaam, Tanzania). Mwaka wa 2014, alipata Shahada ya Uzamili katika sheria za kimataifa na biashara (Master of Laws (LLM) Degree in International Law & International Trade) kutoka St. Augustine University of Tanzania. Mwaka wa 2008-2012, alipata shahada ya kwanza ya sheria, yaani, Bachelor of Law (LLB) Degree (2008-2012) kutoka St. Augustine University of Tanzania.

Kazi na Yanga

Kimsingi anasimamia masuala yote ya kisheria na mipango yanayohusu klabu ya Yanga. Kazi nyingine ni kupitia mikataba ya klabu ya ndani na nje ya klabu, kutunza kumbukumbu za mikataba, kuhakikisha uhuishaji na sheria imeuatwa ipasavyo, kutoa ushauri wa kisheria, tafsiri na miongozo kwa viongozi na maafisa wakuu wa klabu kuhusu mikataba, kupitia taarifa zote na kuandaa utetezi wa kisheria kwa ajili ya matukio yoyote yale ya kisheria dhidi ya klabu na mengine mengi yanayohusu sheria.

Marejeo

  1. YANGA SC YAACHANA NA KATIBU MKUU WAKE, DK DAVID LUHAGO WAKILI SIMON PATRICK KUKAIMU. BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE. Iliwekwa mnamo 2021-11-07.
  2. Yanga suspend acting secretary-general Patrick (en). The Citizen (2020-11-19). Iliwekwa mnamo 2021-11-07.
  3. YANGA SC YAACHANA NA KATIBU MKUU WAKE, DK DAVID LUHAGO WAKILI SIMON PATRICK KUKAIMU. YANGA SC YAACHANA NA KATIBU MKUU WAKE, DK DAVID LUHAGO WAKILI SIMON PATRICK KUKAIMU. Iliwekwa mnamo 2021-11-07.
  4. https://www.dailynews.co.tz/news/2021-06-0360b89f877238c.aspx