Ghurabu (kundinyota) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Add 1 book for verifiability (20211002sim)) #IABot (v2.0.8.1) (GreenC bot
Mstari 9:
Ghurabu lilijulikana kwa jina hili kwa miaka mingi kati ya mabaharia Waswahili waliotumia nyota kutafuta njia baharini wakati wa usiku.<ref>ling. Knappert 1993</ref>
 
Jina la Ghurabu limepokelewa kutoka kwa Waarabu wanaosema <big>الغراب</big> ''al-ghurabghuraab'' na hao walitafsiri jina la Wagiriki wa Kale walioona hapa ndege wa kunguru na kumwita Κόραξ ''koraks''<ref>Jina la Kigiriki "koraks" linaiga sauti ya ndege mwenyewe</ref>, lililotafsiriwa kwa Kilatini kama "Corvus" ambalo ni sasa jina la kimataifa.
 
Katika [[mitholojia ya Kigiriki]] kuna hadithi jinsi gani mungu Apollo alimtuma ndege ya kunguru (Ghurabu) kumchukulia maji kwa bakuli lakini ndege alichelewa kwa sababu alikula matunda njiani. Aliporudi akaeleza kuchelewa kwake kwa uwongo ya kuwa nyoka alimzuia akamwonyesha nyoka kwa kuishika kwenye miguu yake. Apollo alijua ni uwongo akakasirika na kumrusha kunguru (Ghurabu-Corvus) pamoja na bakuli (Batiya-Crater) na nyoka (Shuja-Hydra) kwenye anga wanapokaa kama nyota. Alimwadhibu ndege kwa kuweka bakuli ya maji (Batiya-Crater) karibu naye lakini hawezi kunywa.<ref>Allen, Star-Names and their Meanings uk 180 na [http://www.constellation-guide.com/constellation-list/crater-constellation/ Crater Constellation - Myth], tovuti ya Constellation Guide, iliangaliwa Septemba 2017</ref>