Kobelo Chapombe : Tofauti kati ya masahihisho

Msanii wa Filamu
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '{{Mwigizaji 2 | jina = Kobelo Chapombe | picha = | maelezo ya picha = | jina la kuzaliwa = Emilian Timon Kobelo | tarehe ya kuzaliwa = {{birth date|1987|11|23|mf=yes}} Mwananyamala, Dar es Salaam, Tanzania | mahala pa kuzaliwa = Dar es Salaam | tarehe ya kufa = | mahala alipofia = | jina lingine = Kobelo | kazi yake = Mwigizaji, mtunzi wa hadithi,...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 19:14, 1 Desemba 2021

Emilian Timon Kobelo (amezaliwa 23 Novemba 1987 Mwananyamala, Dar es Salaam) ni mwigizaji, mtunzi wa hadithi, mwongozaji, mhariri wa filamu na mpiga picha kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa uhusika wake wa Kobelo Chapombe ambao hucheza kama mraibu wa pombe.[1]

Kobelo Chapombe
Amezaliwa Emilian Timon Kobelo
(1987-11-23)Novemba 23, 1987 Mwananyamala, Dar es Salaam, Tanzania
Dar es Salaam
Jina lingine Kobelo
Kazi yake Mwigizaji, mtunzi wa hadithi, mwongozaji, mhariri wa taswira mjongeo na mpiga picha
Miaka ya kazi 2002
Watoto 2

Maisha na kazi

Emilian Timon Kobelo ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika famila ya watoto wanne waliozaliwa kati ya Timon Emilian Edward na Christina Stanford Senyagwa. Mwaka wa 2002 alijiunga na kikundi cha sanaa kilichoitwa 'Upendo Art Group.' Alitumikia sanaa ya kwa takribani miaka minne. Mwaka wa 2006, alitoka kundini kisha akajiunga na Baba Watoto Youth Center. Mwaka wa 2008, alishiriki filamu mbili ambazo ziliandaliwa na kundi hilo.

Ilipotimu mwaka 2010, Kobelo na Bakari Salumu walifanya filamu mbili , Giza la Moyo - iliandikwa na Bakari Salumu. 2011 walirudi tena na kazi yao iliyoitwa Wizard of Heart iliandikwa na Kobelo. Kazi hiyo ilisambazwa na Steps Entertainment.

Mwaka wa 2014, alijiunga na kampuni ya Macho Media iliyokuwa chini ya Musa Yusuph Mahenge (Kitale). Akiwa hapa, alipata kushiriki katika filamu ya Shobo Dundo, Nikabu, Kimbiji, Mkubwa Bure, COSOTA, Kigugumizi, Kibena, Stanbakora na Akili.

2017 alishiriki kwenye tamthilia ya Maneno ya Kuambiwa iliyodumu miaka mitatu kupitia kituo cha runinga cha kulipia cha TVE. 2020 ameshiriki kaktika tamthilia ya "Binadamu Wabaya" iliyorushwa hewani kupitia TVE na idhaa ya YouTube maarufu kama IPOTV.

{{BD}1987}}

  1. https://www.youtube.com/watch?v=MzdjBjp9kIo