Mtawa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 13:
Katika [[dini]] mbalimbali, mfano mmojawapo wa [[utawa]] ni ule wa [[wamonaki]]. Lakini katika [[Ukristo]], hasa [[Ukristo wa Magharibi|wa Magharibi]] [[historia ya Utawa]] ilitokeza aina nyingine mbalimbali.
 
==Watawa wa Kanisa Katoliki==
Katika [[Kanisa Katoliki]], mtawa ni [[mwamini]] yeyote aliyejiweka [[wakfu]] kwa [[Mungu]] hasa kwa kushika [[useja mtakatifu]], lakini kwa kawaida pia [[ufukara]] na [[utiifu]].
 
Mara nyingi watawa wanaunda ma[[shirika]] yenye [[karama]] moja inayofafanuliwa na kuratibiwa katika [[kanuni]] na [[katiba]] maalumu.
Line 19 ⟶ 20:
Mtawa anaweza kuwa [[mwanamume]] au [[mwanamke]], mwenye [[daraja takatifu]] au la.
 
Wakristo wote wanavyopaswa kulenga [[Ukamilifu wa Kikristo|ukamilifu]] kutokana na [[amri]] kuu ya [[upendo]], lakini mtawa ana [[wajibu]] wa pekee wa kufanya hivyo kwa kuwa [[adili]] la [[ibada]] linahitaji kuhuishwa na upendo kwa Mungu ulio safi na wa nguvu zaidi na zaidi.
{{mbegu-dini}}
 
Msingi wa wajibu huo ni [[nadhiri za kitawa]], ambazo [[neema]] zake si za [[muda]], bali za kudumu mtu akizidi kuwa mwaminifu. “Wengine wako katika hali ya ukamilifu, si kwa sababu ya kufanya tendo la upendo kamili, bali kwa kujifunga moja kwa moja, kwa fahari fulani, washike kile kinachoelekeza kwenye ukamilifu… Kwa kuwa watawa wanajifunga kwa nadhiri kujinyima malimwengu ambayo wangeruhusiwa kuyatumia kwa hiari; wanafanya hivyo ili kushughulikia mambo ya Mungu kwa urahisi zaidi… Vilevile maaskofu wanajifunga kushika ukamilifu wanapokubali daraja ya uaskofu, kwa sababu mchungaji anapaswa kutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo zake” ([[Thomas Aquinas Mtakatifu|Thoma wa Akwino]]).
 
Mtawa anatamka atalenga ukamilifu: “Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo, kwa ajili yake, nimeshikwa na Kristo Yesu” ([[Waraka kwa Wafilipi|Fil]] 3:12). Hatendi kosa la [[unafiki]] kama hajawa mkamilifu, ila analifanya asipolenga ukamilifu kwa unyofu. Kwake wajibu huo wa pekee na ule wa kushika [[nadhiri]] zake na [[kanuni]] aliyoahidi ni mamoja. Lakini wajibu huo uzingatiwe daima kuhusiana na ule wa jumla unaotokana na amri kuu ya upendo; hapo utawa hautatazamwa upande wa [[sheria]] tu, bali utaonekana katika upana wa maana yake ya Kiroho.
 
Kwa mtazamo huo tu utaeleweka kweli neno zito la Thoma wa Akwino: “Kufanya tendo kwa nadhiri kunastahili kuliko kulifanya bila nadhiri”. Si kwamba tuzidishe nadhiri ili kustahili zaidi, bali mtawa atekeleze nadhiri zake vizuri zaidi na zaidi, akizidi kuchimba sababu tatu alizozitoa mtakatifu huyo katika [[ufafanuzi]] wake:
# Nadhiri ni tendo la adili la ibada, ambalo ni bora kuliko yale ya utiifu, ufukara na usafi wa moyo ambayo linamtolea Mungu yawe ibada.
# Kwa nadhiri ya daima mtu anamtolea Mungu si tendo mojamoja, bali uwezo wenyewe wa kutenda, na kwa hakika ni afadhali kutoa [[mti]] na [[Tunda|matunda]] yake kuliko kutoa matunda tu.
# Kwa nadhiri [[Utashi|utashi]] unaimarishwa katika kutenda mema, na kwa hakika kutenda kwa msimamo kunastahili zaidi, kama vile ni vibaya zaidi kutenda dhambi kwa utashi ulioshupalia [[Uovu|uovu]].
 
Mtu akiishi kwa roho hiyo ataelewa kwa namna hai fundisho la kwamba, kwa kujifunga kushika mashauri matatu, yaliyo [[kiini]] cha utawa, mtu anajitenga na yale yanayoweza yakazuia mapendo yake yasimuelekee Mungu tu, halafu asipofuta uamuzi huo anajitoa kwake kama [[sadaka ya kuteketezwa]]. Hivyo hali yake ni ya kujitenga na [[ulimwengu]] na ya kuwekwa wakfu kwa Mungu.
 
Hasa mambo matatu yanaweza kuzuia mapendo yake yasimuelekee Mungu: [[Tamaa za macho|tamaa za macho]] (yaani za vitu vinavyoonekana), [[tamaa za mwili]] na [[kiburi]] cha maisha (yaani kupenda awe huru tu). Mtawa anayakataa hayo matatu kwa nadhiri zake, akimtolea Mungu [[mali]] kwa ufukara, [[mwili]] na [[moyo]] kwa useja mtakatifu na matakwa yake kwa utiifu. Asipojitwalia tena chochote, bali akitekeleza vizuri, kwa upendo mkubwa zaidi na zaidi, maadili matatu yanayohusiana na nadhiri za kitawa, basi anamtolea kweli Mungu [[sadaka]] ile kamili inayostahili kuitwa ya kuteketezwa. Hapo maisha yake yanatolewa kila siku pamoja na sadaka ya [[misa]] kwa adili la ibada. Ni hivyo hasa kama mtawa anarudia mara nyingi [[ahadi]] zake kwa namna inayostahili kuliko alipozitoa kwa mara ya kwanza. [[Stahili]] zinakua ndani mwake pamoja na upendo na maadili mengine, hivyo hali yake ya kuwekwa wakfu kwa Mungu inazidi kuwa ya dhati na kamili.
 
Lengo la kujinyima pande tatu na kujitoa pande tatu ni kuungana na Mungu kila siku zaidi, kama utangulizi wa [[uzima wa milele]]. Mtawa anaitwa kuufikia muungano huo kwa kumuiga [[Yesu]] aliye “njia, na kweli, na uzima” ([[Injili ya Yohane|Yoh]] 14:6). Yeye, katika ubinadamu wake, alitenganika na roho ya ulimwengu akaunganika na Mungu vizuri iwezekanavyo. Mtawa anatamka hadharani nia ya kumfuata, lakini Yesu alitoka juu, kumbe mtawa ametoka duniani, palipotawaliwa na dhambi, hivyo anapaswa kujitenga zaidi na zaidi na mambo yote ya dunia, kadiri ya maneno haya: “Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu” ([[Waraka kwa Wakolosai|Kol]] 3:1-4). Thoma wa Akwino alifafanua hivi, “Msionje malimwengu kwa kuwa mmefia ulimwengu; uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo; mwenyewe amefichika kwetu, kwa kuwa yuko katika utukufu wa Mungu Baba yake, na hivyo uhai… tulionao kutoka kwake umefichika, kadiri ya maneno ya Maandiko matakatifu, ‘Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako ulizowawekea wakuchao; ulizowatendea wakukimbiliao mbele ya wanadamu!’ ([[Kitabu cha Zaburi|Zab]] 31:19). ‘Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa’ ([[Ufunuo wa Yohane|Ufu]] 2:17)”. Hiyo [[mana]] ya Kiroho, ambayo ile ya [[jangwa|jangwani]] ilikuwa mfano wake tu, ndiyo [[chakula]] cha roho: kujaliwa kuzama katika mafumbo ya imani. Hivyo utekelezaji wa maadili unaandaa kumiminiwa [[sala]]; kwa namna ya pekee “[[Ubikira|ubikira]] unalenga ustawi wa roho katika maisha ya kuzamia sala” (Thoma wa Akwino). Hivyo tena maisha ya kitawa yanalenga zaidi na zaidi utekelezaji kamili wa amri ya upendo na undani wa [[muungano na Mungu]].
 
Wajibu wa pekee alionao mtawa wa kulenga ukamilifu uzingatiwe daima kuhusiana na wajibu wa waamini wote unaotegemea amri kuu ya upendo. Amri hiyo inatawala mashauri ya Kiinjili, kwa kuwa hayo ni njia na vyombo tu kwa ajili ya kufikia ukamilifu wa upendo kwa [[kasi]] na hakika zaidi. Hivyo, maadili matatu ya kitawa yanatekelezwa kikamilifu kwa [[maadili ya Kimungu|maadili matatu ya Kimungu]]. Kati ya hayo yote kuna fungamano la dhati, hivi kwamba [[tumaini]] la [[Heri|heri]] ni kama [[uhai]] wa [[Ufukara|ufukara]] mtakatifu ambao unaachana na mali ya dunia na kutufanya tuzidi kumtumainia Mungu ili kupata ya [[milele]]; upendo ndio uhai wa [[useja]] unaojinyima [[pendo|mapendo]] ya chini ili kupata upendo wa juu kabisa: unapotekelezwa sawasawa unastawisha ndani mwetu upendo kwa [[Bwana]] na kwa watu; imani ndiyo uhai wa utiifu unaotekeleza maagizo ya wakubwa kana kwamba yamefunuliwa na Mungu: utekelezaji huo unakuza roho ya imani. Hivyo maisha ya kitawa yanafikisha kwenye [[sala ya kumiminiwa]] na muungano wa dhati na Mungu unaozidi kustawisha ule na jirani.
{{mbegu-dini}}
[[Jamii:Dini]]
[[Jamii:Ukristo]]