Mzungu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 20:
Asili ya neno haijulikani kikamilifu.
 
Inaonekana kuna uhusiano na neno mzungu / mizungu lisilo kawaida tena katika Kiswahili cha kisasa lakini limetunzwa katika [[kamusi za Kiswahili]] zilizokusanya maneno yao mnamo mwaka 1900. Lilimaanisha mambo mbalimbali kama vile 1) kitu cha ajabu au cha kushangaza, 2) mbinu wa kujiondoa katika tatizo, 3) aina ya [[muhogo]], 4) silika au akili ya wanyama.<ref>kamusi ya [[M-J SSE]] "Mzungu (B)"</ref> Waswahili waliwahi kutumia neno "mzungu" kwa "akili" na pia kwa mafundisho ya "[[unyago]]" yaliyoitwa "kufundishwa mizungu". <ref>kamusi ya Velten, Suaheli Wörterbuch, Suaheli-Deutsch, Berlin 1910, "Mzungu II"</ref>. Kama asili ya "Wazungu" iko hapa iliweza kumaanisha "watu wa ajabu, wasio kawaida, wenye mbinu nyingi" au "wageni walio tofauti sana".
 
Wengine wamehisi kwa utani ya kwamba kuna uhusiano na kitenzi "kuzunguka" na "mzungu" ilitaka kutaja tabia ya wapelelezi, wamisionari na wafanyabiashara wa kwanza kutoka Ulaya ambao hawakukaa mahali pamoja bali kuzungukazunguka kote Afrika.