Tofauti kati ya marekesbisho "Nape Moses Nnauye"

1,924 bytes added ,  miezi 4 iliyopita
kuwa waziri
No edit summary
(kuwa waziri)
'''Nape Moses Nnauye''' ni [[mwanasiasa]] [[Mtanzania]] na mwanachama wa [[chama cha kisiasa]] cha [[CCM]]. Alihudumia kama katibu wa itikadi wa CCM. Amechaguliwa kuwa [[Wabunge wa Tanzania 2015|mbunge]] wa [[Mtama]] kwa miaka [[2015]] hadi sasa. <ref>[http://www.parliament.go.tz/administrations/ Tovuti ya Bunge la Tanzania], iliangaliwa Mei 2017</ref>
 
Aliteuliwa na rais Magufuli kuwa waziri wa habari, utamaduni na michezo. Mwaka 2017 alifutwa uwaziri baada ya kuagiza utafiti wa tendo la [[Paul Makonda]], mkuu wa [[mkoa wa Dar es Salaam]] aliyewahi kuvamia ofisi za kituo cha habari cha kibinafsi cha Clouds<ref>https://theinsider.ug/index.php/2017/03/20/tanzania-government-officials-raid-a-tv-station/ Tanzania government officials raid a TV-station, tovuti ya theinsider.ug, 20.03.2017</ref><ref>https://www.bbc.com/swahili/habari-39416652 Nnauye: Waziri aliyefutwa asema bado anaunga mkono juhudi za Magufuli ; Tovuti ya BBC 28 Machi 2017</ref>. Alipojaribu kujieleza mbele ya wanahabari alizuiliwa na maafisa wa usalama waliotoa bastola na kumwamuru asiseme kitu.<ref>https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/news/nape-s-parting-shot-reveals-deep-divisions-within-govt-2584142 Nape’s parting shot reveals deep divisions within govt; Citizen 24.03.2017</ref><ref>https://www.rfi.fr/en/africa/20170324-tanzania-sacked-information-minister-held-gunpoint-has-no-regrets-about-being-fired Tanzania: Sacked information minister, held at gunpoint has 'no regrets' about being fired, Tovuti ya rfi.fr 24/03/2017; </ref>
 
Baada ya kutokea kwa taarifa kuwa alishiriki katika majidiliano ya kumkosoa rais, kwenye mwaka 2019 alikutana na rais Magufuli akaomba kusamehewa akapata kibali cha rais<ref>https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/news/president-magufuli-s-hand-of-forgiveness-sets-social-media-abuzz-2691590 President Magufuli’s hand of forgiveness sets social media abuzz; Citizen 11.09.2019 </ref>.
 
Katika uchaguzi wa 2020 alirudi bungeni. Kwenye Januari 2022 alirudi kuteuliwa na rais [[Samia Suluhu Hassan]] kuwa waziri wa Wizara ya Habari na Teknolojia ya Habari.<ref>https://www.bbc.com/swahili/habari-59920241 Rais Samia afanya mabadiliko ya baraza la mawaziri na kubuni wizara mpya, Tovuti ya BBC 8 Januari 2022</ref>
 
==Marejeo==