Tofauti kati ya marekesbisho "Chipsi kuku"

2 bytes removed ,  miaka 13 iliyopita
d (CHAKULA MASHUHURI CHIPSI KUKU)
 
== '''CHIPSI KUKU''' ==
 
Karibu kwenye safu maridhawa na leo nalenga moja kwa moja kwa chakula mashuhuri chipsi kuku.
 
Sasa utamaduni wa mswahili kwenye masuala ya maakuli, umemezwa na vibanda vya chipsi kuku katika mitaa mingi ya uswahilini. Chakula cha chipsi kuku kimekuwa mashuhuri, ingawa vipo vingi kama mbatata za urojo (Zanzibar mix). lakini biashara ya chipsi kuku imepanda chati, kwani inavutia wengi hasa kwenye michapuzo ya nguvu ambayo hukolezwa kwenye kilaji hicho cha chipsi kuku kama tomato sosi , chili sosi, rojo zito zito la embe mbichi au ukwaju na pilipili juu yake. Watafutaji ajira hamkani katika harakati za kuwaridhisha wateja wao, na wateja nao wake kwa waume humiminika kujipatia huduma hiyo, Alhamdulilah tumbo halilali na njaa.
 
Mandhari ya biashara hizi hutofautiana kutokana na vipato vya watafutaji ajira, kuna sehemu ambazo utastarehe na kiyoyozi juu yake, lakini sehemu nyengine kutokana na mazingira yake, fumba macho tu kama una njaa au waswahili wanasema ‘usimchungue kuku atakushinda kumla ‘. Lakini yote kenda , kumi mmeyaona mafuta yanayochomewa chipsi kuku ? Ikiwa kwenye karai au fraya. Haya mafuta yakipelekwa kwa mkemia mkuu sijui atatujibu nini. Hivi haya maradhi si ya kujitakia ? hatukatai chipsi kuku zisiuzwe lakini haya mafuta jamani mtatuuwa kwa maradhi ya kansa , mbali na maradhi hayo mapumzi juu juu na matumbo kama wajawazito.
6

edits