Mizizi ya dhambi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Rescuing 2 sources and tagging 0 as dead.) #IABot (v2.0.8
No edit summary
Tag: Disambiguation links
 
Mstari 18:
| year = 1997
| origyear = 1997-10-23 }}</ref> zote zikitokana na [[umimi]] usiozingatia [[ukweli]].
 
==Asili==
Mizizi ya dhambi, yaani [[majivuno]], [[uzembe]], [[kijicho]], [[hasira]], [[uroho]], [[utovu wa kiasi]] na [[uzinifu]], si dhambi kuu kuliko zote; lakini ndivyo vilema tunavyovielekea kwanza na ndivyo vinavyotusogeza zaidi mbali na [[Mungu]] na kututumbukiza katika makosa makubwa zaidi, k.mf. [[uzushi]], [[Uasi|uasi]] wa [[dini]], kukata tamaa na kumchukia Mungu. Mtu hafikii uovu mkubwa mara moja, bali polepole, akiteleza kwenye mteremko.
 
Ni muhimu tutafiti kwanza asili yenyewe ya mizizi saba ya dhambi. Yote inatokana na kujipendea, yaani umimi unaotuzuia tusimpende Mungu kuliko yote. “Kujipendea ni chanzo cha kila dhambi” ([[Thomas Aquinas Mtakatifu|Thoma wa Akwino]]). “Mapendo mawili yamejenga miji miwili: kujipenda hadi kumdharau Mungu kumejenga mji wa Babuloni; kumbe kumpenda Mungu hadi kujidharau kumejenga mji wa Mungu” ([[Augustino]]).
Tunampa kisogo kwa sababu tu kwa kujipendea tunataka mambo kinyume na [[sheria]] yake. Basi, tunatakiwa [[ufishaji|kufisha]] hiyo asili ya dhambi zote ili tujipende kitakatifu: ndio tendo la pili la [[upendo]], ambalo tunajipenda kwa ajili ya Mungu, ili kumtukuza sasa na [[milele]]. Mwenye [[dhambi ya mauti]] anajipenda kuliko yote, hata kuliko Mungu. Kumbe mwadilifu anampenda Mungu kuliko [[nafsi]] yake, halafu anapaswa kujipenda ndani ya Mungu na kwa ajili ya Mungu; anapaswa kuupenda [[mwili]] wake ili usaidie [[roho]], badala ya kuzuia [[uhai]] wake wa juu; anapaswa kuipenda roho yake ili aishi milele kwa uzima wa Kimungu; anapaswa kupenda [[akili]] yake na [[utashi]] wake ili vizidi kuishi kwa [[mwanga]] na upendo wa Mungu.
 
Kujipendea ndio chanzo cha mambo yale matatu yanayotokeza wazi roho ya ulimwengu kuhusu mwili, [[mali]] na roho. Dhambi za mwili zinatia aibu kuliko zile za roho, kwa kuwa zinatushusha kwenye ngazi ya [[Mnyama|wanyama]]; lakini zile za roho (k.mf. [[kiburi]]), ambazo peke yake zinapatikana ndani ya [[shetani|mashetani]], ni mbaya zaidi, kwa kuwa zinapingana na Mungu na kutusogeza mbali naye zaidi.
 
[[Tamaa]] za mwili ni kupenda pasipo utaratibu [[Kitu|vitu]] vinavyofaa kudumisha uhai wetu binafsi na wa ubinadamu kwa jumla; [[pendo]] hilo lisiloratibiwa linasababisha utovu wa kiasi na uzinifu. Hivyo uchu unaweza ukawa [[miungu|mungu bandia]] na kutupofusha zaidi na zaidi.
 
Tamaa za macho ni kupenda pasipo utaratibu vile vinavyopendeza [[Jicho|macho]]: umaridadi, [[utajiri]], hasa [[pesa]] inayowezesha kujipatia chochote. Ndipo unapotokea uroho unaofanya [[hazina]] yetu iwe mungu wetu tukiiabudu na kuitolea [[sadaka]] [[muda]], [[nguvu]], [[familia]], hata [[uzima wa milele]].
 
Kiburi cha maisha ni kupenda pasipo utaratibu ukuu wetu, yale yote yanayoweza kutukuza, hata kama ni magumu. Anayefuata hicho kiburi, mwishowe anajiabudu kama shetani. Ndipo zinapoweza zikatokea aina zote za dhambi, halafu upotovu wa milele. Kiburi si mmojawapo tu kati ya mizizi ya dhambi, bali ni asili hasa ya vilema vinne vifuatavyo: majivuno, uzembe, kijicho na hasira. Majivuno ni kupenda pasipo utaratibu sifa na [[heshima]]. Uzembe unahuzunikia kazi ya kulenga [[Utakatifu|utakatifu]] kwa sababu inadai [[Juhudi|juhudi]] na kujikana. Kijicho kinatufanya tusikitikie mema ya wenzetu, kwa kuwa yanaonekana kuzuia ukuu wetu. Hasira isiyoratibiwa (si ya [[haki]]) inatufanya tupinge kwa nguvu yale yasiyotupendeza. Vilema hivyo - hasa uzembe, kijicho na hasira - vinazaa [[huzuni]] mbaya inayogandamiza roho, kinyume cha [[amani]] na [[furaha]] zinazotokana na upendo.
 
[[Mbegu]] hizo zote za [[mauti]] tunapaswa kuzifisha, si kuziratibu tu: kwanza umimi, unaozaa hayo matatu yanayosababisha mizizi saba ya dhambi: “Kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi” ([[Waraka kwa Waroma|Rom]] 8:13). [[Ukweli]] huo unaonekana wazi katika maisha ya watakatifu, ambapo [[neema]] inakuja kutawala mielekeo yote ya [[umbile]] lililoanguka ili kuliponya na kulishirikisha uhai bora zaidi. Haja hiyo ni wazi kwa roho ya [[Kikristo]], na utekelezaji wake wenye [[bidii]] unaandaa kutakaswa na Mungu kwa ndani zaidi ili kuangamiza viini vya kifo vilivyobaki bado katika [[Hisi|hisi]], akili na utashi.
 
==Matokeo==
Mizizi ya dhambi inaitwa hivyo kwa sababu ni vyanzo vya vilema vingine. Hivyo majivuno yanazaa [[ukaidi]], [[majigambo]], unafiki, ushindani, kupenda mapyamapya, [[ubishi]]. Hayo yanaweza yakafikisha kwenye maanguko mabaya zaidi na uasi wa dini. Uzembe au ukinaifu kuhusu mambo ya Kiroho unapingana moja kwa moja na upendo wa Mungu na kuzaa uovu wa moyo, [[kinyongo]] au [[ukali]] kwa jirani, kutotaka kuwajibika, kukata tamaa, [[usingizi]] wa roho, kusahau [[amri]] na kutafuta yaliyokatazwa. Wakiteleza kwenye mteremko huo wa kiburi, majivuno na uzembe, wengi wamepoteza [[wito]] wao. Kijicho kinazaa [[chuki]], [[masengenyo]], [[masingizio]], furaha kwa mabaya yanayowapata wengine na huzuni kwa mafanikio yao. Utovu wa kiasi na uzinifu vinazaa [[upofu]] wa roho, [[ugumu wa moyo]], kushikilia maisha haya hata kupotewa na [[tumaini]] la uzima wa milele, kujipendea hata kumchukia Mungu, hatimaye kutotubu wakati wa kufa.
 
Mara nyingi mizizi hiyo ni dhambi za mauti, ila ni nyepesi ikiwa jambo husika ni dogo au [[hiari]] inapolichagua si kamili. Inaweza kupatikana kwa namna ya chini, kama inavyowatokea wengi wenye [[Dhambi ya mauti|dhambi za mauti]], lakini inaweza pia kuwemo ndani ya watu wenye neema inayotia utakatifu kama namna za upotovu wa [[Maisha ya kiroho|maisha ya Kiroho]]: k.mf. kiburi kuhusu maisha ya Kiroho kinatufanya tukwepe wanaotukosoa, hata kama wana haki na [[mamlaka]] ya kufanya hivyo, halafu tuwe na kinyongo nao; [[ulafi]] kuhusu maisha ya Kiroho unaweza ukatutamanisha [[Faraja|faraja]] za kihisi katika [[sala]], hata tuzitafute kuliko Mungu. Hiyo miwili pamoja inasababisha [[njozi]] bandia n.k.
 
Tofauti na maadili, vilema havishikamani, tena vingine havipatani: hivyo tunaweza kuwa na kimoja pasipo vingine. Hata hivyo tunapaswa kutekeleza maadili mengi, kama [[arubaini]], ambayo karibu kila mojawapo ni [[kilele]] kati ya vilema viwili vinavyopingana. Tena, kasoro kadhaa zinafanana na maadili kwa namna fulani: basi, ni muhimu tuwe na [[Upambanuzi|upambanuzi]] ili kuvitofautisha, la sivyo katika [[Piano|kinanda]] cha maadili tutatoa [[Nota nzima (muziki)|noti]] zisizotakiwa, tukidhani uzembe ni [[unyenyekevu]], ukali ni haki, udhaifu ni [[huruma]].
 
==Kujitafiti==
Orodha hiyo ya matunda mabovu ya kujipendea inatuelekeza kujitafiti na kukubali [[upana]] wote wa ufishaji unaohitajika ili tuishi kwa dhati uzima halisi. Kwa kuwa ukweli wa miguso yetu haueleweki kwa urahisi, tunapaswa kujitafiti wa makini. Kazi hiyo, badala ya kuondoa mawazo yetu yasimuelekee Mungu, iturudishe kwake mfululizo. Tunapaswa kuomba mwanga wake ili tujione kidogo anavyotuona yeye au tutakavyojiona [[Hukumu ya mwisho|siku ya hukumu]]. Kila [[jioni]] tutafiti kwa unyenyekevu na majuto makosa tuliyoyafanya kwa mawazo, maneno, matendo na kutotimiza [[wajibu]]. Lakini tusizidishe kwa kutafuta makosa madogo mno hata tukahangaishwa na kusahaulishwa mambo muhimu zaidi. Lengo si kuorodhesha kikamilifu makosa, bali ni kuona kwa [[Unyofu|unyofu]] chanzo chake ndani mwetu. Ili kuponya [[upele]], hatuwazi kuponya vijipu kimojakimoja, bali kusafisha [[damu]]. Tusisimame mno kujitazama hata tukaacha kumkazia macho Mungu, bali tujiulize mbele yake anatuonaje. Ndivyo tunavyoona masharti matakatifu ya [[dhamiri]] ya Kikristo, yanayopita yale ya [[mwanafalsafa]] yeyote. Tusitenganishe kamwe makosa na huruma isiyo na mipaka, bali tuyaone katika mwanga wa [[wema]] wa Mungu ulio tayari daima kusaidia. Hivyo [[utafiti]] hautasababisha tukate tamaa, bali utazidisha tumaini letu kwake.
 
Kuona makosa yetu kunatuonyesha pia [[thamani]] ya maadili yaliyo kinyume chake. Tunathamini haki hasa tunapoonja uchungu wa kukosewa haki. Ubaya wa uzinifu utuonyeshe thamani ya [[usafi wa moyo]]; vurugu za hasira na kijicho zitufanye tuthamini [[Upole|upole]] na upendo halisi; uharibifu unaotokana na uzembe uchochee ndani mwetu hamu ya juhudi na furaha ya Kiroho; upotovu wa kiburi ututambulishe [[hekima]] na ukuu wa unyenyekevu halisi.
 
Tumuombe [[Bwana]] atutie chuki takatifu kwa dhambi, kwa kuwa dhambi inatuondolea wema mkuu wa Mungu aliyetujaza [[Fadhili|fadhili]] za ajabu na anayetuahidia nyingine za thamani zaidi tukidumu kuwa waaminifu. Kwa namna fulani chuki hiyo ni upande wa pili wa upendo kwa Mungu. Haiwezekani kupenda ukweli pasipo kuchukia [[uongo]], wala kumpenda Mungu pasipo kuchukia yanayotusogeza mbali naye. Watakatifu wanyenyekevu na wapole wana chuki takatifu kwa uovu iliyo na nguvu sawa na upendo wao kwa Mungu. Tujiombee chuki hiyo dhidi ya kiburi na vinginevyo ili upendo halisi kwa Mungu na kwa watu uzidi kustawi ndani mwetu. Njia ya kushinda kiburi ni kuzingatia mara nyingi [[Yesu]] alivyodhalilishwa, pamoja na kujiombea unyenyekevu. Ili kuzima kijicho tumuombee jirani yale tunayojitakia. Tujifunze pia kuzuia mara hasira ikipanda kwa kusogea mbali na kile kinachoisababisha, pamoja na kuzoea kutenda na kusema kwa upole. Ufishaji huo ni wa lazima. Ili tuendelee kuelekea [[Ukamilifu wa Kikristo|ukamilifu]], tufikirie [[Malipizi|malipizi]] ya watakatifu, tukizingatia kuwa sisi pia tunatakiwa kufia dhambi zaidi na zaidi kwa ustawi wa maadili yote, hasa upendo.
 
==Tanbihi==
Line 43 ⟶ 73:
* [http://www.paintedchurch.org/deadlysi.htm Medieval mural depictions] - in parish churches of England (online catalog, Anne Marshall, Open University)
* [https://www.smashwords.com/books/view/397532 ''Stranger'', An Allegorical Tale of the Seven Deadly Sins] {{Wayback|url=https://www.smashwords.com/books/view/397532 |date=20140714153927 }}, ISBN 9781311073846
 
{{mbegu-dini}}
 
[[Category:Maadili]]
[[Category:Ukristo]]