Ukanamungu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa umeelekezwa kwenda Ukanaji Mungu
Tag: New redirect
 
Removed redirect to Ukanaji Mungu
Tag: Removed redirect
 
Mstari 1:
[[Picha:Professor_Richard_Dawkins_-_March_2005.jpg|thumb|right|200px|[[Profesa]] [[Richard Dawkins]] ni mwatheisti mashuhuri wa karne ya 21.]]
#REDIRECT[[Ukanaji Mungu]]
'''Ukanamungu''' (pia: '''Uatheisti''' kutoka [[neno]] la [[Kiyunani]] cha kale, ''atheos'', likiwa na maana ya "bila miungu") kijumla ni msimamo wa kutokuwa na [[imani]] juu wa uwepo wa [[miungu]], ama kukataa imani kuwa kuna miungu, yaani ni dhana kuwa hakuna [[Mungu]] wala miungu. Hivyo ni kinyume cha Utheisti, imani kuwa angalau kuna Mungu mmoja.
 
[[Asili]] ya neno Uatheisti, limechipuka hata kabla ya [[karne ya 5]], lilitumika kuwakilisha wale wasioamini uwepo wa miungu inayoabudiwa na [[jamii]] kubwa ya [[Binadamu|watu]], wale waliovunjwa mioyo na miungu, au wale wasioona sababu yoyote ya msingi ya kuamini uwepo wa miungu.
 
Neno lenyewe uatheisti lilianza kutumika hasa mnamo [[karne ya 16]], baada ya kusambaa kwa fikra huru dhidi ya [[dini]].
 
Watu wa kwanza kujitambulisha kama waatheisti, waliishi [[karne ya 18]] wakati wa [[Zama za Mwangaza]]; [[mapinduzi ya Ufaransa]] yalishuhudia vuguvugu kubwa la kisiasa kuwahi kutokea kwenye [[historia]], lililotetea ukuu wa fikra za binadamu.
 
[[Hoja]] zinazotetea uatheisti, zimegawanyika kwenye makundi mbalimbali yakiwemo ya kifalsafa, kijamii na kihistoria.
 
[[Mantiki]] ya kutoamini uwepo wa miungu inajumuisha, tatizo la [[uovu]], hoja ya [[ufunuo|funuo]] zinazokinzana, na kukataa [[dhana]] isiyoweza kupingika.
 
Wasioamini wanadai kuwa uatheisti ndio dhana asili ya binadamu kuliko Utheisti, kwa sababu kila mtu anazaliwa bila kuwa na imani ya Mungu au miungu; kwa maana hiyo basi, ni [[Wajibu|jukumu]] la anayeamini uwepo wa miungu au Mungu kuthibitisha madai yake na si jukumu la atheisti kuthibitisha kuwa hakuna Mungu au miungu.
 
[[utafiti|Tafiti]] za zamani kutoka shirika la habari la Uingereza ([[BBC]]), zilionyesha kuwa 8[[Asilimia|%]] ya watu wote [[duniani]] ni waatheisti, huku zile za zamani zaidi zikionyesha kuwa ni 2% pekee, na wale wasiokuwa na dini yoyote wakiunda 12% ya watu wote duniani.
 
[[Mwaka]] [[2015]], tafiti zimeonyesha 61% ya watu wa [[China]] walikuwa waatheisti, huku tafiti za mwaka 2010 zikionyesha kuwa 20% ya watu wa [[Umoja wa Ulaya]] hawaamini uwepo wa [[roho]] ya aina yoyote wala miungu, huku [[Ufaransa]] na [[Uswidi]] zikiongoza kwa [[idadi]] kubwa ya waatheisti, zikiunda 40% na 34% kila mmoja.
 
==Tafsiri na Aina==
Uatheisti ni dhana inayokanusha uwepo wa miungu. Mara nyingi aina mbili za ukanamungu hutofautishwa ambazo ni:
* ukanaji unaosema hakuna sababu ya kuamini kuwepo kwa Mungu kwa sababu [[akili]] au [[sayansi]] zinaweza kueleza kila kitu.
* ukanaji mkali unaodai ya kwamba kuwepo kwa Mungu hakuwezekani.
 
Wakanaji mashuhuri wa [[karne ya 19]] walikuwa [[Ludwig Feuerbach]], [[Karl Marx]], [[Friedrich Engels]], [[Arthur Schopenhauer]] na [[Friedrich Nietzsche]]. Wakanaji muhimu katika [[karne ya 20]] walikuwa kwa mfano [[Stephen Hawking]], [[Siegmund Freud]], [[Bertrand Russell]], [[Albert Camus]], [[Simone de Beauvoir]], [[Louis de Broglie]], [[Erwin Schrödinger]], [[David Kellogg Lewis]], [[Vladimir Lenin]], [[Paul Dirac]], [[Marlene Dietrich]], [[Albert Einstein]], [[Jean Baptiste Perrin]], [[Mao Zedong]], [[Auguste Comte]], [[Noam Chomsky]], [[Isaac Asimov]], [[James Chadwick]], [[John Lennon]], [[David Attenborough]], [[Michel Foucault]], [[Richard Feynman]], [[Niels Bohr]], [[Douglas Adams]], [[Christopher Hitchens]], [[Daniel Dennett]], [[Richard Dawkins]], [[Sam Harris]], na [[Umberto Eco]].
 
==Viungo vya Nje==
* [http://www.iep.utm.edu/n-atheis Kuhusu Wakanaji Mungu wapya kwenye ''The Internet Encyclopedia of Philosophy'']
* {{dmoz|Society/Religion_and_Spirituality/Atheism/|Mambo mbalimbali kuhusu Ukanaji Mungu}}.
* [http://www.bbc.co.uk/religion/religions/atheism/ Dini na Maadili—Ukanaji Mungu kwenye tovuti ya BBC]
* [http://www.infidels.org/library/ Maktaba ya mtandaoni kuhusu Ukanaji Mungu]
* [https://www.ted.com/talks/richard_dawkins_on_militant_atheism Video ya Richard Dawkins akihutubia kuhusu Ukanaji Mungu]
* [https://www.youtube.com/watch?v=y8hy8NxZvFY Video ya mdahalo kuhusu Ukanaji Mungu]
{{mbegu-dini}}
[[Jamii:Dini]]
[[Jamii:Falsafa]]