Iwiji : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 18:
 
}}
'''Iwiji ''' ni jina la [[kata]] ya [[Wilaya ya Mbeya Vijijini]] katika [[Mkoa wa Mbeya]], [[Tanzania]]. Wakati wa wa [[sensa]] iliyofanyika [[mwaka]] [[2012]], kata ilikuwa na wakazi wapatao 9049<ref>{{Cite web |url=http://www.meac.go.tz/sites/default/files/Statistics/Tanzania%20Population%20Census%202012.pdf |title=Sensa ya 2012, Mbeya - Mbeya DC |accessdate=2017-03-12 |archiveurl=https://web.archive.org/web/20040102080416/http://www.meac.go.tz/sites/default/files/Statistics/Tanzania%20Population%20Census%202012.pdf |archivedate=2004-01-02 }}</ref> walioishi humo. [[Msimbo wa posta]] ni 53213.
 
Kuna vijiji vya Iwiji, Isende na Izumbwe II.
 
==Kijiji cha [[Izyira==]] kimepewa hadhi ya kuwa kata inayojitegemea mwaka [[2014]].
Kijiji cha Izyira kimepewa hadhi ya kuwa kata inayojitegemea mwaka [[2014]] ikiwa imetokea baada ya kugawa kata ya Iwiji ambapo mwanzo kijiji hiki kilikuwa kipo kata ya Iwiji. Kijiji hiki kinapakana na kijiji Ibezya cha [[wilaya ya Ileje]] kusini mashariki, kusini kinapakana na [[Wilaya ya Mbozi]] vijiji vya Hezya na kijiji cha cha Namwangwa na kuendelea mpaka magharibi kijiji cha Haraka na Idiwili kaskazini kuna kijiji cha Iwiji na safu ya milima Mbeye na mlima Makungulu iliyoambatana na msitu Mang'onga na msitu Mbogho.
 
Misitu hii ni muhimu kwa kuwa ndicho chanzo kikuu cha mito mikuu mitatu ambayo ni Mto Magole, Mto Salaga na Mto Mafumbo. Mito hii ndio chanzo pekee ambayo inashikilia asilimia 85% ya kilimo cha umwangiliaji wa vijiji vyote katika ukanda wa vijiji vyote vilivyovitajwa hapo juu kuwa jirani ya Izyira.
 
Izyira hukaliwa na makabila matatu ya [[Wanyiha]], [[Wandali]] na [[Wamalila]]. Kijiji hiki kuna mila na desturi zake kikiongozwa na mila za kijadi. Kiongozi akiitwa mwene wa ukoo wa Mwazembe. Kati ya Wakristo kuna hasa madhehebu yaliyo kwenye jumuiya ya CCT. Kijiji hiki kina shule tatu. Izyira ni shule mama iliyoanzaishwa mnamo miaka ya [[1957]] kwa mfumo wa shule za TAPA iliyoanza na mwalimu mzawa Winfred Mtindo Mwazembe baadaye zilianzishwa shule mbili kutokana na ongezeko la watu ambazo ni Mwenge na shule ya msingi Masewe. Pia wananchi katika mfumo wa kila kata kujenga shule ya sekondari kijiji kama kijiji walijenga shule ya sekondari ya kijiji kwa mpango wa kijitolea pamoja na kuwa na shule ya sekondari ya kata ambayo ipo makao ya kata pale Iwiji pia mwaka 2009 shule ya sekondari ilifunguliwa katika kijiji cha Izyira mwezi April 29 chini ya mkuu wa shule Godlove Ngonde
 
Kijiji hiki kinahudumiwa na barabara kuu kutoka mbalizi ikipitia vijiji vifuatavyo mbalizi Izumbwe I, Mganjo, Isangati Santilya, Shipongo, Ilembo, Italazya, Shigamba, Izumbwe II. Iwiji barabara inagawanyika, kushoto inakwenda makao makuu ya Wilaya ya Ileje yaani Itumba na kulia barabara hii ndiyo inakwenda moja kwa moja Izyira hatimaye huendelea Wilaya ya Mbozi kupitia vijiji vya Hezya, ,Nyimbili, Ilengo, Shumba, Hasamba na kuungana tena na barabara kuu ya Dar es Salaam mpaka Zambia pale makao mkuu ya Wilaya ya Vwawa.
 
Chakula chao kikuu kinatokana na mazao yaani mahindi, ndizi na viazi vitamu. Zao la biashara ni kahawa. Mito mitatu hupitia kijiji hiki, mto Magole upo mashariki sambamba na kijito kidogo kiitwacho Itaga katikati kuna kijito kingine Salaga magharibi kuna mto mkubwa Mafumbo na magharibi kuna kijito kingine shongo. Mito yote hii ndio chanzo kikuu cha uzalishaji wa chakula cha wakazi wa kijiji cha Izyira na vijiji vya jirani mito hii mkubwa miwili yaani Magole na Mafumbo ikisaidiana na vijito hivi hutiririsha maji mwaka mzima. Muungano wa mito hii miwili hufanya mto mmoja unaokwenda kusini kupitia karibu sana na Itumba kuungana na [[mto Songwe]] ulio kama mpaka wa Tanzania na Malawi. Kuna milima mkubwa mitatu kaskazini ambayo ni Mlima Mbeye, kaskazini magharibi Mlima Makungulu na magharibi kuna Mlima Mwira. Katika milima hii kuna misitu minene ambayo ndio maji ya mito hii huanzia katika misitu hiyo.
Kutokana na ongezeko la watu misitu hii miaka ya karibuni kumekuwa na uharibifu mkubwa na kusababisha mito hii kupungua sana tena sana kwa ujazo wa maji na kusababisha kupungua kwa kiwango cha unyeshaji wa mvua, kama hatutakuwa na mkakati wa kuzuia uharibifu huu wa misitu hii msitu Mang'onga na msitu Mbogho upo uwezekano wa mito hii kukauka na kusababisha hali mbaya kwa vijiji vyote vinavyopata huduma ya maji ya mito hii mikubwa si IZYIRA tu hata WILAYA jirani kama ILEJE na Mbozi.
 
Kijiji hiki, pamoja na kuwa na vitongoji kumi vinahudumiwa na zahanati moja tu.
Kata ya Izyira ina Jumla ya vitongoji vinne ambavyo ni Izyira, Masewe, Inuka na Mapita ikiwa ni kijiji kilichotokea baada ya kugawa kijiji cha Izyira
 
Mwaka 2014 kijiji cha Izyira kilipata hadhi ya kuwa kata yaani kata ya Izyira ambayo ina vijiji vitatu na vitongoji tajwa hapo juu imeweza kuingizwa kwenye mradi wa kujenga kituo cha afya kwenye kata hiyo. Kituo hiki kinajengwa katika eneo la kitongoji cha Inuka eneo hili ni eneo ambalo liko katikati ya kata hii ya Izyira lakini pia eneo hili linalojengwa kituo cha afya lina historia yake pamoja na kuwa katikati ya kata ya Izyira.
 
Eneo hili ndipo ilipoanzishwa shule ya kwanza kabisa enzi kabla hata nchi hii haijapata Uhuru ya pata miaka 70 iliyopita ,hivyo nj jambo la busara kwa uamuzi uliotolewa na kikao kilichofanya maamuzi hayo kulienzi eneo hilo japo watu wengi hawajui nini maana ya kujenga kituo katika eneo hilo.
 
Ninatoa pongezi za dhati kwa uongozi wa wilaya ya Mbeya kuona kuwa ni vyema kujenga kituo cha [[afya]] katika kata hii kwa kuwa kama ujenzi huu utakamilika ni msaada mkubwa kwa ukanda huu wa [[kusini]] mwa wilaya ya Mbeya vijijini kuwa na huduma hii ya Kituo cha AFYA kwa sababu kata hii wananchi wajke walikuwa wana pata shida sana hasa akina mama na watoto wanapohitaji huduma ya matibabu ilikuwa inawalazimu kusafiri umabali mrefu kupata matibabu kwani iliwalazimu kwenda wilaya ya Ileje, ama kwenda na kusafili umbali wa kupata matibabu hospitali ya Mkoa wa Songwe ambayo zamani ilikuwa ni hospital ya wilaya ya Mbozi katika mji wa Vwawa ama hospitali ya binafasi ya Mbozi mission.
 
Kituo hiki kinajengwa kwa nguvu za wananchi na mpaka sasa kipo hatua ya kujenga msingi asilimia kubwa ya [[ujenzi]] wa kituo hiki nai nguvu za wananchi kwa kuwa hujitolea matofali ,mawe,mchanga na mafundi ambapo shughuli hii inaendeshwa kwa njia inayoitwa mpango wa (nguvu kazi) maendeleo yanayofanyika kila Jumanne ya kila wiki ................nitaendelea kuwalete taarifa zaidi kila ninapopata jipya katika akaunti yangu mimi Moja Kazimoto Kabenga wengine walizoea kuniita mwangalanani kazimoto kabenga
 
==Marejeo==
{{marejeo}}
{{Kata za Wilaya ya Mbeya Vijijini}}
 
{{mbegu-jio-mbeya}}
 
[[Jamii:Mkoa wa Mbeya]]
[[Jamii:Wilaya ya Mbeya Vijijini]]