Raila Odinga : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 15:
== Elimu na kazi ==
Raila baada ya kumaliza shule nchini Kenya alikwenda kusoma [[uhandisi]] katika Chuo cha Ufundi [[Magdeburg]] ([[Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani]]) kati ya [[1965]] hadi [[1970]]. Alipata digrii ya MSc kama mhandisi. Alijiunga na [[Chuo Kikuu cha Nairobi]] kama mwalimu hadi 1974 alipokuwa naibu mkurugenzi katika [[Shirika la Viwango Kenya]] (Kenya Bureau of Standards).
[[Picha:Raila Amolo Odinga - World Economic Forum on Africa 2008.jpg|thumb|Odinga mwaka 2008.]]
Raila alianzisha makampuni kadhaa kama vile Applied Engineering Services na Pan African Petroleum Limited. Ameendelea kuendesha kampuni ya familia ya Spectre International Limited inayoshika 40% za hisa za kiwanda cha ethanol cha Kisumu na East African Spectre inayotengeneza chupa za gesi ya kupikia. Mwaka [[2007]] alikadiriwa kuwa na mali yenye thamani ya takriban bilioni 4 za shilingi za Kenya.