Mizimu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d Masahihisho aliyefanya 2A03:2880:31FF:71:0:0:FACE:B00C (Majadiliano) yalirejeshwa hadi sahihisho la mwisho na 31.59.82.231
Tag: Rollback
No edit summary
 
Mstari 1:
'''Mizimu''' inamaanisha hasa [[roho]] zilizoishi katika [[mwili]] kabla ya kuiaga [[dunia]].
 
Katika baadhi ya [[dini]] na [[mila]] inaaminika kuwa mizimu inaweza kuwa na [[faida]] kwa watu waliopowalio hai duniani na ina uwezo wa kuwasiliana nao kwa kutumia njia mbalimbali kufuatana na [[mazingira]] au [[utamaduni]].
 
Kuna tofauti kati ya mizimu; pengine ni roho za [[binadamu]] ambao hawakutimiza [[Wajibu|majukumu]] yao au walifanya kinyume wakati wapo duniani; pengine ni roho za watu walioshi kwa [[Adili|uadilifu]].
 
Katika [[Kanisa Katoliki]] na baadhi ya [[madhehebu]] mengine, mizimu inaweza kuwa ya [[watakatifu]].
 
==Mizimu katika jadi za Afrika==
Kuna tofauti kati ya mizimu; pengine ni roho za [[binadamu]] ambao hawakutimiza majukumu yao au walifanya kinyume wakati wapo duniani.
Watafiti mbalimbali walioangalia jamii za jadi katika [[Afrika]] walikuta [[imani]] katika mizimu. Imani hizo hazitokei Afrika tu, maana imani za kufanana zilitambuliwa pia katika [[dini za jadi]] katika [[Bara|mabara]] mengine kama vile [[Asia]] na [[Ulaya]]. Lakini kila [[jamii]] ina namna yake ya pekee ya kuwaza na kushughulikia imani hizo.
 
Kwa [[lugha]] ya [[Kiswahili]], "mzimu" ni [[neno]] linalotaja pia mahali ambapo watu huwasiliana na roho za watu waliofariki dunia zamani.
 
Tena baadhi ya jamii za Kiafrika huamini kuna mizimu iliyoumbwa katika hali hiyo, yaani haikuwahi kuwa binadamu hapo kwanza.
 
Kwa hiyo, kuna imani ya mizimu ya aina mbalimbali: mizimu ambayo ni roho za watu waliokufa na mizimu ambayo haijawahi kuwa binadamu.
Kwa kuwa mizimu ni roho, haina [[umbo]] maalumu, lakini ina uwezo wa kutokea katika [[Umbile|maumbile]] tofautitofauti kama vile mtu, [[mnyama]], [[mdudu]], [[Mmea|mimea]], au vitu visivyo na [[uhai]].
 
Kwa [[utamaduni]] [[utamaduni wa Kiafrika|wa Kiafrika]], mizimu mizuri ni wahenga, yaani roho za watu ambao walipokuwa katika hali ya ubinadamu waliishi vizuri kulingana na tamaduni na matakwa ya jamii, walikuwa na sifa nzuri. Sasa ni mizimu mizuri ambayo hulenga kuilinda jamii au mtu mmojammoja dhidi ya matatizo. Hivyo, pale mtu anapokumbwa na matatizo wahenga humsaidia. Aidha, kufanikiwa au kutokufanikiwa kwa jamii katika masuala mbalimbali kunatokana na uhusiano wao na wahenga. Jamii inapaswa kufuata mila na [[desturi]] zake na kuepuka, kadiri iwezekanavyo, kuvunja [[Mwiko|miiko]] ya jamii kwa sababu kufanya hivyo kunawaudhi wahenga. Mtu anayefuata kanuni zote hulindwa, hupata mafanikio na kuishi kwa [[amani]] ilhali yule anayekiuka mila na desturi hupatwa na majanga makubwa au anaweza kuiingiza jamii nzima katika matatizo kwa sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wahenga kujitoa katika [[ulinzi]] na hivyo kuyaachia mizimu mibaya nafasi ya kufanya mambo mabaya, au wahenga wenyewe kutoa [[adhabu]] kwa jamii au kwa mtu mmojammoja.
 
Aidha, inasadikiwa kuna mizimu mibaya, ambayo malengo yao ni kuidhuru jamii na wakati mwingine hujitokeza kama pepo ambao huwaingia na kuwadhuru watu; hao huitwa kwa [[jina|majina]] tofautitofauti kama vile misoha, irumenang, na’ndenga na war’umu kwa [[Wabena (Tanzania)|Wabena]], [[Wamasai]], [[Wamakonde]] na [[Wachagga|Wachaga]]. Baada ya [[Uislamu]] na [[Ukristo]] kuenea barani Afrika [[kusini kwa Sahara]] yanatumika pia majina yanatokana na lugha ya [[Kiarabu]] kama [[shetani|mashetani]] au [[Jini|majini]] ambayo kwa [[asili]] yana maana tofauti. Hao mizimu mibaya huwa na kinyume cha sifa hizo hapo juu, yaani walipokuwa binadamu waliishi katika hali isiyotakiwa katika jamii au inayochukuliwa kuwa ni ya kutia [[aibu]], halafu kufa katika hali inayochukuliwa kuwa ni ya [[laana]], kama vile kujinyonga au kuzikwa bila kufuata mila na desturi za jamii. Kwa mfano, [[Wanyore]] wa [[Kenya]] huamini kuwa [[Mwanaume|mwanamume]] au [[mwanamke]] anayefariki dunia kabla hajaoa au kuolewa atataka kuzuia wengine kuoa au kuolewa na kuzaa. Kwa hiyo, kabla ya miili ya wanaume na wanawake hao kuzikwa, inafanyiwa miviga ili kuzuia tatizo hilo lisienee kwa wengine. Aidha, inasadikiwa kuwa baadhi ya mizimu mibaya hutokana na [[Mtoto|watoto]] ambao walikufa kabla ya kuzaliwa: hao huidhuru jamii kwa sababu huwa na [[hasira]] na hutaka kulipa [[kisasi]].
 
{{mbegu-dini}}