Majina ya kisayansi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
 
Mstari 11:
Mifano mashuhuri ni kitabu cha "Species Plantorum" (Aina za mimea) cha [[Carl Linne]] kilichoandikwa kwenye mwaka [[1753]] kwa Kilatini na kuwa msingi wa [[uainishaji wa kisayansi]] katika biolojia hadi leo.
 
==Majina ya sayansi katika biolojia==
Utaratibu wa [[uainishaji]] wa [[wanyama]] na [[mimea]] ulioanzishwa na [[Carl Linnaeus]] unaendelea kufuatwa hadi leo, hivyo kila mmea au mnyama anapewa jina la kisayansi yenye sehemu mbili: sehemu ya kwanza inataja [[jenasi]] na sehemu ya pili [[spishi]]. Kwa kawaida jina la mnyama linafuatwa na jina la [[ukoo]] (au [[kifupi]] chake cha [[herufi]] kadhaa) la [[mtaalamu]] aliyewahi kueleza spishi hiyo katika [[Maandishi|maandiko]] ya [[sayansi|kisayansi]], pamoja na [[mwaka]] ambapo makala yake imetolewa. Jina la mmea linafuatwa na kifupi cha herufi moja au kadhaa cha jina la mtaalamu bila mwaka. Majina ya jenasi na spishi huandikwa kwa mlazo na lile la jenasi linaanzia na herufi kubwa.