Adili : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 51 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q157811 (translate me)
No edit summary
Tag: Disambiguation links
 
Mstari 1:
[[Picha:Efez Celsus Library 2 RB.JPG|thumb|300px|Sanamu ya adili (kwa [[Kigiriki]] ''ἀρετή'') huko [[Efeso]], [[Uturuki]]]]
'''Adili''', (kutoka [[neno]] la [[Kiarabu]]; kwa [[Kiingereza]] "virtue" kutoka [[Kilatini]] ''virtus'', yaani nuguvu) ni uzoefu wa kutenda kiutuvema.
 
==Katika falsafa==
Huko [[Ugiriki]] katika [[karne ya 5 K.K.]] [[Mwanafalsafa|wanafalsafa]] [[Plato]] na hasa [[Aristotle]] waliorodhesha maadili mengi yanayotegemea [[nne]] za msingi ([[maadili bawaba]]): [[busara]], [[haki]], [[nguvu (adili)|nguvu]] na [[kiasi]]. Zaidi ya hayo, walionyesha kwamba haiwezekani kujipatia adili moja tu, bali uadilifu unadai mtu awe na maadili yote. Kwa mfano, haiwezekani kuwa mtu wa haki pasipo busara.
 
==Katika Ukristo==
Katika [[Ukristo]], juu ya [[maadili ya kiutu]], mwamini anatakiwa kupokea [[maadili ya Kimungu]] yaliyoorodheshwa na [[mtume Paulo]], yaani [[imani]], [[tumaini]] na [[upendo]] ambayo yanaendana vilevile. Mtu anatakiwa kulenga [[ushujaa]] katika maadili yote.
 
===Ushujaa wa maadili kwa jumla===
Ushujaa wa maadili, unaodaiwa na [[Kanisa]] ili kutangaza [[mtumishi wa Mungu|watumishi wa Mungu]] kuwa [[Mwenye heri|wenye heri]] [[Mbingu|mbinguni]], unaanza katika [[Matakaso ya Kimungu|utakaso wa Kimungu]] wa [[Hisia|hisi]] yanapopatikana matendo ya kishujaa ya [[usafi wa moyo]] na ya [[subira]]. Matendo ya kishujaa yanapatikana zaidi katika [[usiku wa roho|utakaso wa Kimungu wa roho]] unaoingiza katika [[hatua ya muungano]], na hasa baada ya jaribu hilo. Tukimuona mtu ametoka [[handaki]] hilo la kwanza, na zaidi hilo la pili, akiwa na ushujaa wa maadili, ni [[dalili]] ya kuwa amevuka vizuri asiache [[njia]]; au, kama alitenda makosa, ameinuliwa tena na [[neema]] ya [[Mungu]] na kuletwa hadi [[unyenyekevu]] mkubwa zaidi, kwa kutojiamini na kumtegemea yeye tu.ù
 
====Sifa za adili la kishujaa====
“Adili la kawaida linamkamilisha [[binadamu]] kiutu, kumbe adili la kishujaa linampatia [[Ukamilifu wa Kikristo|ukamilifu]] upitao utu. [[Shujaa]] akiogopa penye sababu za kuogopa, ni adili; asingeogopa katika nafasi za namna hiyo angekuwa shupavu tu. Lakini asipoogopa tena kitu kwa sababu anategemea msaada wa Mungu, adili hilo linapita utu, ni la Kimungu” (Thoma wa Akwino). Juu kuliko maadili ya [[raia]] mwema, mtakatifu huyo alifafanua maadili yanayotakasa: “Ni yale ya watu wanaoelekea kufanana na Mungu. Hapo busara inadharau malimwengu yote ipende zaidi kuzama ndani ya Mungu na kuelekeza mawazo yote kwake; kiasi kinaachana na madai ya [[mwili]] kadiri [[umbile]] linavyoweza kuvumilia; nguvu inamzuia mtu asiogope [[Mauti|kifo]] wala [[ahera]]; hatimaye haki inamsukuma ashike moja kwa moja njia hiyo ya Kimungu tu”. Juu ya hayo tena yapo maadili ya roho iliyokwishatakata, yaani yale ya [[Mtakatifu|watakatifu]] wakuu hapa [[Dunia|duniani]] na ya wenye heri mbinguni: “Hapo busara ni kama inahisi mambo ya Kimungu; kiasi hakijui tena [[tamaa]] za kidunia; nguvu inasahaulisha [[hofu]] yoyote; haki inafunga na Mungu [[agano]] agano la [[milele]]”. Akizungumzia [[Heri Nane]] alisema kuwa ndiyo matendo ya juu zaidi ya maadili na ya [[vipaji vya Roho Mtakatifu]], na kuwa [[tuzo]] yake hapa duniani ni utangulizi fulani wa heri ya milele.
 
Mafundisho kuhusu adili la kishujaa yalijumlishwa hivi na [[Papa Benedikto XIV]], “Masharti manne yanatakiwa kwa adili la kishujaa lililothibitishwa au lililodhihirika: 1) jambo linatakiwa kuwa gumu, la juu kuliko nguvu za kawaida za watu; 2) linatakiwa kutendwa mara, kama kwa urahisi; 3) tena kwa [[furaha]] takatifu; 4) si kwa nadra, bali kila inapopatikana nafasi”. Hivyo ushujaa wa maadili ni wa juu kuliko kawaida ya waadilifu. Unajitokeza mtu anapotimiza [[Wajibu|majukumu]] yote bila wasiwasi wala shuruti, hata katika nafasi ngumu zaidi.
 
Masharti hayo yaeleweke kuhusiana na mtu anayetekeleza adili la kishujaa: lililo gumu kwa [[mtoto]] wa miaka kumi ni lile lipitalo nguvu za kawaida za watoto wenye [[umri]] wake; vilevile lililo gumu kwa [[mzee]] ni tofauti na lililo gumu kwa mtu mwenye [[afya]] na nguvu. La pili, yaani utayari na urahisi, lieleweke upande wa juu wa [[roho]], bila kukanusha ugumu upande wa chini, fumbo la [[Getsemane]] linavyothibitisha; ili [[sadaka]] ya kuteketezwa ikamilike ni lazima uwepo [[uchungu]] na ugumu mkubwa unaoshindwa mara na upendo wa kishujaa. Vilevile furaha takatifu, iliyo sharti la tatu, ni ile ya sadaka inayotupasa, nayo haizuii uchungu wala [[huzuni]], bali pengine inaendana na hali ya kukaribia kulemewa ambayo inatolewa kitakatifu kwa Mungu; tena furaha ya kuteseka pamoja na [[Bwana]] inaongezeka pamoja na uchungu, ndiyo sababu ni dalili ya neema kubwa. Sharti la nne, yaani mazoea ya kutenda hivyo nafasi ikipatikana, linathibitisha zile zilizotangulia na linaonyesha adili la kishujaa lililokwishajaribiwa kweli.
 
Ushujaa wa maadili unadhihirika hasa katika [[Mfiadini|kifodini]], lakini hata nje ya hapo, k.mf. katika kusamehe na kupenda kwa namna ya ajabu wadhalimu. Ndivyo ilivyomtokea kwa namna ya pekee [[Yesu]], hata kabla ya [[Msalaba wa Yesu|mateso yake]], alivyoonyesha hasa kwa upendo wake usio na mipaka kwa ajili ya wote, upendo wa [[mchungaji]] aliyejiandaa kutoa [[uhai]] wake kwa ajili yetu.
 
Katika adili la kishujaa [[wastani]] adili ni wa juu kuliko katika adili la kawaida: sasa adili linatekelezwa pamoja na kipaji kinachohusiana nalo, na kwa kuwa linatumikia upendo tunakuta ndani yake mruko wa adili hilo la Kimungu. Halafu, kwa kuwa matendo ya kipaji yanategemea [[uvuvio]] wa [[Roho Mtakatifu]], Mkristo shujaa anadumu mnyenyekevu kama [[mwana wa Mungu|mtoto wa Mungu]] anayemtazama daima [[Mungu Baba|Baba]], tofauti na shujaa anayezingatia nguvu zake mwenyewe na kulenga makuu yatakayomtukuza, kuliko kumuacha Bwana atawale kwa dhati ndani mwake.
 
====Ushujaa na ulinganifu wa maadili====
Ili tutofautishe uadilifu wa kishujaa, unaotokana na msaada mkubwa wa Mungu, na mambo yanayoonekana tu kufanana nao, tunapaswa kuzingatia masharti hayo manne lakini pia [[ulinganifu]] wa maadili. Busara, [[dereva|dreva]] wa maadili, inaongoza maadili ya kiutu, wakati upendo unaelekeza matendo ya maadili yote kwa Mungu na kuyafanya yastahili. Ndiyo sababu maadili yote, yakiunganika katika busara na upendo, yanakua pamoja kama [[Kidole|vidole]] vitano vya [[mkono]] uleule mmoja, au kama [[viungo]] mbalimbali vya mwili mmoja. Fundisho hilo ni la msingi ili kubainisha maadili ya kishujaa, kwa sababu kutekeleza kwa pamoja maadili yanayoonekana kupingana kuna ugumu wa pekee, kwa kuwa [[silika]] ya kila mmojawetu inaelekea adili moja au lingine. Maadili ya kujipatia na ya kumiminiwa yanatakiwa kukamilisha maelekeo mema ya umbile letu na kupinga kasoro zinazoliharibu. Tunapaswa kupiga [[Piano|kinanda]] bila kutokeza [[Nota nzima (muziki)|noti]] zisizolingana na nyingine, tusichanganye [[upole]] na [[woga]], wala [[moyo mkuu]] na [[kiburi]].
 
Basi, tunaona umuhimu wa ulinganifu wa maadili, na ugumu wa kuyatekeleza yote karibu kwa [[wakati]] mmoja ili kudumisha ulinganifu wa [[maisha]] maadilifu. Litokanalo ni kwamba adili lolote halina kiwango cha ushujaa ikiwa mengine hayapo katika kiwango hichohicho walau katika utayari wa roho kuyatekelezwa nafasi ikidai hivyo. Si busara kutamka haraka kuwa mtumishi wa Mungu ana ushujaa wa adili fulani halafu kufasiri kwamba kwa sababu hiyo anayo mengine pia kwa kiwango hicho; ili tuweze kusema adili mojawapo ni la kishujaa, ni lazima tuwe tumeshapima ukuu wa mengine. Ingawa maadili, hasa ya Kimungu, yanakua pamoja, fulani anaweza kuelekea kiumbile au kimazoea adili moja au lingine; tena kuna watumishi wa Mungu ambao, kwa ajili ya [[utume]] maalumu, wanapokea [[neema za msaada]] zinazowafanya watekeleze adili moja kuliko mengine.
 
Mungu tu, anayeunganisha ndani mwake [[sifa]] zote kamili, anaweza kuwajalia watumishi wake waunganishe vilevile maadili yote katika mwenendo wao. Ulinganifu wa ajabu wa maadili ulionekana hasa ndani ya Bwana wakati wa mateso, ambapo tunaona upendo wa kishujaa kwa Mungu na [[huruma]] isiyopimika kwa watesi pamoja na upendo mkuu kwa ukweli na haki; unyenyekevu wa dhati na moyo mkuu wa ajabu; nguvu ya kishujaa katika kujishusha na upole mkuu. Hivyo ubinadamu wa [[Mwokozi]] ni [[kioo]] safi ambamo sifa za Mungu zinarudisha [[mwanga]] wake.
 
Ulinganifu wa maadili ndio unaotofautisha [[Mfiadini|mashahidi]] wa kweli na watu waliovumilia mateso kwa kiburi na ushupavu katika kushikilia udanganyifu. Mashahidi wa kweli tu wanaunganisha nguvu na upole unaowafanya wawaombee watesi wao kama alivyofanya Mwokozi. Hasa ndani mwao tunakuta masharti manne ya uadilifu wa kishujaa tuliyoyafafanua. Humo tunaona kazi maalumu ya Mungu anayetegemeza watumishi wake asiache kuwajalia neema za pekee katika nafasi ngumu zaidi.
 
Tusisitize kuwa ushujaa wa watoto unapimwa kulingana na nguvu za kawaida za watoto waadilifu wa umri uleule. Ikiwa [[watu wazima]] kadhaa uadilifu wao ni mdogo, wapo watoto ambao uadilifu wao ni mkubwa. “Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao umeiweka misingi ya nguvu; kwa sababu yao wanaoshindana nawe” ([[Kitabu cha Zaburi|Zab]] 8:2). Yesu aliwakumbusha maneno hayo [[kuhani|makuhani]] na [[Mwandishi|waandishi]] waliochukizwa na watoto kushangilia, “Hosana, [[Masiya|Mwana wa]] [[Daudi (Biblia)|Daudi]]!” ([[Injili ya Mathayo|Math]] 21:15). Ikiwa pengine imani ya watoto ni kielelezo kwa watu wazima, ni vilevile kuhusu tumaini lao na upendo wao. Tukisoma matendo ya kishujaa ya watoto wenye umri wa miaka kumi na miwili au chini ya hapo, na maneno mazuri ajabu ambayo baadhi yao waliyatamka kabla hawajafa, tunakuta [[hekima]] ambayo katika usahili na unyenyekevu wake ni ya juu kuliko [[elimu]] changamano ya kibinadamu. Ni kipaji cha hekima katika kiwango cha juu, kulingana na upendo wa hao watoto ambao ni wakubwa kwa ushuhuda wa kishujaa waliomtolea Mungu. Katika usafi wa mtoto aliyebatizwa Roho Mtakatifu hahitaji kutakasa mengi kabla hajamshirikisha mianga yake na nguvu zake. Bila shaka mna [[donda|madonda]] ya [[dhambi ya asili|dhambi asili]] ambayo baada ya [[ubatizo]] ni kama [[kovu|makovu]] yanayoelekea kupona; lakini hayana [[sumu]] inayotokana na makosa yaliyorudiwarudiwa kwa [[hiari]]. Mtoto akiwa mwaminifu kwa neema katika kutimiza wajibu wa umri wake, Roho Mtakatifu anamsamehe matakaso yale machungu ambayo kwa waliotenda [[dhambi]] ni ya lazima kadiri walivyopotea. Hapo mtoto anainuka hata juu.
 
[[Jamii:Maadili]]