Majadiliano:Ukristo : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
dNo edit summary
 
Mstari 101:
 
:Sawa kipala... Tupo pamoja !--[[User:Moses|Moses]] 15:41, 24 Juni 2007 (UTC)
 
==Makala hii ya sasa==
 
Nimepitia ukurasa huu leo na kukuta masahihisho mengi ambayo nadhani hayapendezi hasa kuwa jarida la watu wote kusoma na
 
kupokea hivyo na changamoto ya mjadala.
 
Ukristu ni dini kuu ya ulimwengu, ikiwa na wafuasi zaidi ya bilioni mbili (taz. Dini); kitabu chake kitakatifu kinajulikana
 
kama Biblia.
 
-Kuusema ukristu kwa msingi wa ufafanuzi wa takwimu za idadi ya waumini na kuuita ni dini kuu hakusaidii kumfanya mdadisi
 
aelewe ukristo ni nini. Kwa kweli takwimu zina sehemu yake. Lakini katika mfumo huu mpya wa jukwaa la maarifa vijana na
 
watoto wetu wanapenda kujua kinaga ubaga kuhusu dini mbali mbali na hivyo ni vema tukaweka habari za kiufundi za kiuchunguzi
 
ili kusaidia ufahamu na maarifa ya kizazi chetu na kijacho wanaofanya chaguo sahihi la kujitambua kwa chocote kile
 
wanachojisikia kwa wakati kuhusiana nacho. Jukwaa hili lijitahidi kuepuka mlengo wa kuuza picha ya mtu aliye ndani(mwenye
 
maslahi na hoja); ni vema kila mchangiaji ajipime ikiwa anachangia toka nje ama ndani. Ikiwa yuko ndani basi awe tayari
 
kukosolewa na aliye nje. Lakini mchangiaji bora kabisa ni yule mwenye kuona ndani na lakini akasema toka nje na ingawaje
 
anauelewa mpana na hata zaidi ya somo lenyewe. Hii italeta mseto bora ambao ndio hasa; makala ambazo watu wa leo na wale
 
waliokatika kusaka zaidi hutafuta.
 
yaani Mpakwamafuta (Kristo kwa Kigiriki),
-Kristo husemwa pia kuwa ni mpaka mafuta, lakini hili ni swala mjadala katika jukwaa la teolojia. Maana kuna mengi sana humo.
 
Lakini ieleweke kuwa teolojia zote zina mapengo yake. Na baadhi ya hayo mapengo yanaweza kutafutiwa majawabu tokea kwenye
 
vyanzo mbalimbali, hata hapa kwenye wikipedia; ni uwanja mmoja mmojawapo ambao wengine wapo tayari kutoka huo mchango. Kwa
 
mfano, neno mesiya lina mizizi sawa na neno 'mashaikh' la kiebrania kuwa na maana ya mwenyekutwaa watu(kitu) toka kwenye
 
vingi... Sasa aliyetoa neno kristu toka kwenye kigiriki afanye utafiti zaidi atakuta na hili. Ndio maana kabla makala hii
 
haijaandikwa hivi. Mesiya ilifafanuliwa kimkato na neno Mkombozi.
 
Musa, mwanamapunduzi aliyewakomboa watu wa Israeli kutoka utumwani Misri takribani miaka 1250 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu
 
-Musa alikuwa ni mwanamatengenezo(Social Reformer, samahani kuleta lugha ya kigeni), mapinduzi yana sura ya kupindua madaraka
 
na kuinua mapya na pia kubadili mifumo ya kijamii... Musa alikomboa na kujaribu kusimamisha upya msingi ya kijamii kwa
 
Torati. Na hivyo haya ni matengenezo ambayo ni tafsiri sanifu ya neno reformations(tena, samahani)
 
 
 
Maana Ya Kristo,
 
-Aya zote zilizo chini kichwa hichi cha habari hazitoshelezi kufafanua:- Ifahamike kuwa sisi wote tupo katika kujifunza na
 
kuongeza nuru yetu katika kuyajua na kuyafahamu mambo yahusiyo Ukristo; hivyo kristo kama neno ama hali ni vema kufafanuliwa
 
ili kuwa mtu yeyote; hata ambaye hajapata kusikia kuhusu ukristo aweza kusoma na kupata picha halisi. Sasa aya yote iliyobaki
 
pale chini huzungumza juu ya 'mystical knowing'(Kujua kwa jinsi ya ndani, jinsi ya kiroho). Na katika hili ifahamike kwamba
 
Imani ni kuwa na Hakika. Mafundisho yote ya nje ya dini kulenga katika kumuongoza mwenye kuanza kwa kusadiki afike mahala,
 
roho yake itaanzamfunza na kumjenga na kuwa taa yake. Mwongozo huu wa kiimani ni 'kernel' ya dini zote; na ndiyo chenye
 
kuitwa IMANI hasa. Hiyo dini ni mafundisho ya nje ya mwongozo; pia kusema mapokeo(mfano wa palilizi). Lakini Imani ndiyo
 
tunda lenyewe. Kuna ufundi ambao dini zote zaweza kuelezwa kufika katika shina hili lenye kuunganisha lugha ya nje iliyopo
 
katika dini zote na Kilicho hasa hasa katika undani wa mtu. Na jukwaa hili la wikipedia ni uwanja wetu wa kufanya hili
 
kuwezekana. Inawezekana kabisa mtu hajawahi kabisa kudhania hili, lakini ni hivyo. Kilicho muhimu ni watu kuwa nia moja
 
kusaidia kushiriki upeo wa kuona na kuwakilisha.
 
Mafarakano Makuu Kati ya Wakristo
 
-Badala ya kuelezea ya mafarakano; ni bora zaidi kueleza kilicho kiini halafu kumulika ni jinsi gani vingine huchipukia. Ndio
 
maana makala ya mwanzo ililenga kueleza kiini. Historia ni mchakato wa nje katika nyakati. Ina sehemu yake. Lakini zama hizi
 
kuna uwezekano kabisa kutenganisha Historia na sayansi ya metamofosia ya kiroho ambayo dini zote hunyooshea kidole. Na hapa
 
kwenye hili jukwaa ni ukumbi mmoja wapo wa kufafanua hivi vyote viwili na hata kuvibainisha. Ingelikuwa ni bora makala zote
 
za dini ziwe sura mbili zenye kuchambuliwa moja ni ya kihistoria na ingine ni kuchambuliwa kwa kiini cha uasili
 
mbegu(essence) cha mafundisho yake kwa msaada wa moja kwa moja wa yale yalisemwa katika maandiko yake ili kuunganisha Mtu na
 
Manani(The Divine). Nalo hili lawezekana kabisa.
 
Utabiri wa kuja kwake ulianzia katika bustani ya Edeni pale Mungu alipomwambia mwanamke "uzao wako utamponda kichwa" nyoka,
 
yaani shetani
 
-Katika maandiko ya dini mbali mbali kuna visa vya masimulizi vyenye kubeba mafumbo ya kiroho(Allegories) ambayo ni vema
 
kutochukuliwa kijuu juu tu kwani mengi ya hayo hupwaya katika mizani ya sura halisi ya mambo. Hii ndiyo yenye kuleta hali ya
 
wengi kupuuzia mafundisho ya dini mbali mbali na kuyaona ni upuuzi ama mambo magumu kueleweka kwa mtu wa kawaida. Basi ni
 
vema kutoka michango yenye mantiki iliyowekwa wazi kumulika dhana maelezo. Na vile vile ni jukumu la kila mtu kusahihisha ama
 
kukosoa pale ambapo mwingine anaonekana kama kwamba anaichukulia mifano kama hiyo kwa juu juu. Na pia kutafuta michango zaidi
 
kuboresha picha.
 
Naomba kuwakilisha hoja.
 
Ni hayo tu
 
mengine yatafuatia baadaye
 
--[[User:Moses|Moses]] ([[User talk:Moses|majadiliano]]) 17:21, 26 Aprili 2008 (UTC)
Return to "Ukristo" page.