Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1:
'''Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki''' ([[Kijerumani]]: Deutsch-Ostafrikanische Gesellschaft (DOAG)) ilikuwa shirika ya binafsi iliyoundwa na [[Karl Peters]] ikaanzisha koloni ya [[Afrika ya Mashariki ya Kijerumani]].
 
==Mikataba ya ulinzi na machifu wa Tanganyika==
''(kwa habari za undani tazama [[Karl Peters#Peters alianzisha Afrika ya Mashariki ya Kijerumani]])<br>''
Ilianzishwa kwa jina la "Shirika kwa koloni za Kijerumani" mwaka 1884. Wawakilishi wake walisafiri mwaka uleule Zanzibar na kuingia Tanganyika barani. Walitembelea machifu kadhaa upande wa mashariki wa maeneo chini ya utawala wa Zanzibar kwenye pwani. Hapa waliongea vizuri na machifu wakawaambia ya kwamba mfalme mkubwa huko Ulaya anawapenda yu tayari kuwasaidia dhidi ya maadui na pia dhidi ya Wazanzibari. Waliombwa kukubali urafiki na mfalme mkubwa wa [[Berlin]] na kutia sahihi mikataba ya urafiki na ulinzi. Machifu kadhaa walitia sahihi kwenye mikataba yaliyoandikwa kwa Kijerumani bila kuelewa walichofanya wala yaliyomo ya mikataba ile. Maneno ya mle yalisema ya kwamba chifu anakabidhi nchi yake yote kwa kampuni pamoja na haki za matumizi na haki za mali ya ardhi, biashara na kodi.
 
==Barua ya ulinzi kutoka serikali ya Ujerumani==
Peters alikataliwa awali na serikali ya [[chansella]] [[Bismarck]] ambaye hakuona faida ya kuunda koloni akaogopa hasara. Lakini Peters aliitisha serikali ya kwamba angeweza kuuza maeneo yale kwa mfalme [[Leopold II wa Ubelgiji]] aliyejenga wakati uleule koloni yake katika Kongo. Hapa Bismarck aliogopa wanasiasa katika bunge waliowahi kudai koloni za Ujerumani eti wangesema kwa nini mtu mwema anayetaka kutupatia koloni amedharauliwa na sasa wageni wa Ubelgiji wamepata faida. Hivyo Peters alipewa barua ya ulinzi kutoka serikali ya Berlin iliyosema ya kwamba maeneo yote yaliyotajwa katika mikataba yako chini ya Ulinzi wa serikali ya Ujerumani.
 
==Uenezaji kwenye pwani na anguko==
''(kwa habari za undani angalia [[Karl Peters#Mwisho wa himaya ya Peters na shirika la koloni]])<br>''
[[1888]] kampuni ilikodisha pwani lote la Tanganyika ya baadaye kutoka [[Zanzibar]]. Jaribio lake la kulitawala hali halisi kuanzia [[15 Agosti]] 1888 likasababisha ghasia na [[vita ya Abushiri]].