Mkataba wa Helgoland-Zanzibar : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 4:
 
==Shabaha ya Mkataba==
Shabaha kuu ya mkataba ilikuwa kuondolewa kwa hatari za magongano kati ya Ujerumani na Uingereza. [[Leo von Caprivi]] alikuwa [[chansella]] mpya wa Ujerumani tangu Machi 1890 akimfuata [[Otto von Bismarck]]. Caprivi alitaka kujenga uhusiano mwema hasa na Uingereza.
 
Wakati huohuo uhusiano ule ulikuwa mashakani kidogo kutokana na matendo ya [[Karl Peters]] aliyejaribu kupanusha eneo la [[Shirika la Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki]] hadi [[Uganda]] kinyume cha mapatano ya mwaka 1886 kati ya Ujerumani na Uingereza juu ya mipaka ya maeneo chini ya athira yao katika [[Afrika ya Mashariki]].