Biblia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
wale jamaa wa Christodelfian wametupa maandiko yao humo ovyo
Mstari 1:
{{kidhehebu}}
 
'''Biblia''' ni jina la jumla kwa ajili ya vitabu vitakatifu vya dini ya [[Uyahudi]] na hasa ya[[Ukristo]]. Neno limetokana na lugha ya [[Kigiriki]] ambayo ndani yake '''βιβλία''' ''biblia'' ina maana ya "vitabu" ikiwa ni uwingi wa βιβλος ''biblos''. Hii ni kwa sababu Biblia ni mkusanyo wa maandiko mbalimbali yaliyoweza kutungwa kwa muda wa miaka 1000 hivi.
 
Line 9 ⟶ 11:
 
''Unabii wa Biblia:''
 
'''UTHIBITISHO KWAMBA MUNGU YUPO'''
 
Biblia ni kitabu cha ajabu kuliko vyote. Maelezo yake kuhusu chanzo cha uovu; taarifa yake isiyo na kasoro kuhusu mahusiano ya Mungu na taifa la Israel; ujumbe wake unaopenya kupitia kwa manabii wao; ‘habari njema’ yake iliyohubiriwa na Yesu Kristo na mitume wake; na juu ya yote uchambuzi wake sahihi uhusuo mapungufu ya silka ya mwanadamu ukilinganishwa na utakatifu, kweli na rehema ya Mungu, iliyodhihirishwa zaidi hasa katika Mwanawe - haya yote ni mambo ya kipekee yasiopatikana katika kitabu kingine chochote duniani. Haya yalimfanya Henry Rogers, miaka 100 iliyopita kusema: “Biblia sio namna ya kitabu ambacho mwanadamu angekuwa ameandika kama angeweza, au angeweza kuandika angeweza”. Kwa maneno mengine, Mungu anahitajika katika kuelezea uwepo wake.
 
Mstari 17:
 
'''NANI MWENYE MAMLAKA YA UNABII?'''
 
Lakini kwanza inabidi tukubaliane juu ya swali moja la muhimu: Biblia inadai kwamba mamlaka ya unabii inatoka kwa Mungu tu na ni uthibitisho wa uweza wake?
 
Line 43 ⟶ 42:
 
'''BIBLIA INATABIRI YAJAYO?'''
 
Tunaweza tu kuchunguza historia na uzoefu wetu kutambua kwamba wanadamu kwa jinsi walivyo, hawawezi kujua hata kidogo ya mbeleni. Kwa nini? Hatuwezi hata kujua litakalotupata usiku wa leo, au kesho tukienda kazini, achilia mbali mwaka kesho; au litakaloipata dunia katika miaka 100, hata tusiposemea miaka 2000! Watu wangekuwa na utambuzi kidogo tu wa mambo yajayo, maamuzi mengi yangebadilika kiasi gani! Ajali nyingi kiasi gani zingeepukwa! Maafa mengi kiasi gani yasingeliachiwa yatokee. Vita vingi kiasi gani visingeanzishwa! Uzoefu katika maisha yetu wenyewe, na wa historia ya mwanadamu unatuonyesha kuwa mwanadamu hana ufahamu wowote wa hakika wa litakalotokea.
 
Line 63 ⟶ 61:
 
'''UNABII KUHUSU BABELI'''
 
Katika enzi ya manabii wa Israeli (Kama 850-560 K.K) kuliinukia dola mbili kuu katika maeneo yanayoizunguka mito ya Frati na Tigrisi, katika Iraki ya sasa. Ya kwanza ilikuwa dola ya Ashuru iliyokuwa na makao makuu Ninawi. Kwa karne mbili, Waashuru walivamia ardhi ya mataifa waliowazunguka: kusini wakawatawala Wakaldayo na makao makuu yake Babeli; Magharibi wakaikalia Shamu, na kuendelea chini katika pwani ya Bahari ya Kati, kupitia Israeli mpaka Misri. Sera yao ilikuwa ya kigaidi. Lengo lao lilikuwa kuwatisha wakazi wa maeneo hayo watii na kulipa kodi kwa mwaka. Kufanikisha hili waliiswaga miji kiuporaji na kuichoma moto, wakavibamiza vijiji, na kuua wakazi na kuchukua maelfu ya mateka Ashuru.
 
Line 73 ⟶ 70:
 
'''MAANGUKO KAMILI'''
 
La ajabu, miaka 100 kabla Babeli haijafikia kilele cha ukuu wake, nabii Isaya alishatabiria kuangushwa kwake kwa maneno thabiti sana. Katika kifungu kilichopewa kichwa cha habari ‘Mzigo wa Babeli’ ni hivi alivyosema.
 
Line 99 ⟶ 95:
 
'''HATIMA YA MISRI'''
 
Misri iliwahi pia kuwa dola yenye nguvu kubwa katika Mashariki ya Kati. Ukubwa wake ulikuwa kama 1600 (K.K) wakati majeshi ya Mafarao wavamizi walipojisogeza kusini ndani ya Sudani, Magharibi kuambaa pwani ya Afrika ya kaskazini, kaskazini kupita ardhi ya Kaanani (baadaye Israeli), na ndani ya Syria. Uvumbuzi kaatika baadhi ya Mahekalu ya kale, minara na makaburi umedhihirisha utukufu wa Mafarao ulivyokuwa katika kilele cha kuu wao.
 
Line 111 ⟶ 106:
 
'''Ufalme mdogo'''
 
Na ndivyo ilivyotokea. Tangu kama mwaka 600 K.K, Misri aliangukia chini ya watawala wa kivamizi, kwanza wa Wababeli katika karne ya 6 K.K; kisha Waajemi kati ya karne ya 6 na 4; alafu Wayunani katika karne ya 4; wakifuatiwa na Warumi karne ya kwanza K.K mpaka karne ya 5 B.K. Walifuatiwa na Waarabu na Waturuki kutoka karne ya 7 B.K na kuendelea. Hata Waingereza wameitawala Misri kwa kipindi katika karne ya 19. Kwa miaka 2500, Misri imebakia kama alivyotabiri Ezekiel kuwa ingekuwa, “Ufalme wa chini,” wakati wote ikikaliwa na wengine. Lakini Misri na Wamisri hawakutokomea. Bado wapo, na wameponea uhuru kiasi miaka ya karibuni, washukuru misaada mikubwa ya fedha wanayopata kutoka Marekani na Saudi Arabia.
 
Line 117 ⟶ 111:
 
'''UNABII KUHUSU ISRAELI'''
 
Huu ndio uliojaa kuliko wote, kimaelezo ya utabiri wake, na pia katika wingi wa thibitisho zihusuzo ukweli wake kimatukio kihistoria. Tutazingatia tu mambo halisi mepesi yahusuyo hatima ya ajabu ya Waisraeli.
 
Line 160 ⟶ 153:
 
'''Nani angeweza kujua?'''
 
Utabiri wa mambo wa muda mrefu hivyo unawezekanaje? Kuna jibu moja tu linaloridhisha; Lazima awepo aliyeyajua kabla; lakini ni nani? Kwa hakika hakuna mtu wa miaka 2500 iliyopita au tangu hapo, angeweza kujua. Tukiupima utabiri wa namna hii kibinadamu tu hauelezeki. Lakini hata hivyo, manabii wa Agano la Kale hawakudai wanatabiri kwa uwezo wao. Walisema walikuwa wakisema maneno yaliyotoka kwa Mungu. “ Hivi ndivyo asemavyo BWANA,” ndivyo walivyokuwa wakianza kusema wakati wote. Kama Mungu alikuwa nyuma ya yale waliyosema, tunapata jibu la nani aliyejua.’ Hakuna maelezo mengine yanayoleta maana. Unabii tuliouchunguza hapa ulihitaji uwepo wa Mungu kama chanzo chake. Inaleta maana.
 
Line 168 ⟶ 160:
'''BIBLIA NA MATAIFA'''
 
Unabii wa Daniel unao mpango wa kuvutia unaohusu kukua na kuanguka kwa dola, na hali ya mataifa ya kile kilichokuwa kikiitwa ‘Dunia iliyostaarabika,’ yaani mataifa ya Ulaya, Mashariki ya Kati, Misri na pwani ya kaskazini mwa Afrika, yote yanayoizunguka Bahari ya Kati (Mediterranean sea). Unabii huu ulitolewa wakati Daniel alipokuwa mateka katika boma Babeli karne ya 6 K.K. Ukweli wake umejidhihirisha katika historia tangu siku hizo hadi sasa.
 
Line 189 ⟶ 180:
 
'''Mungu anayefunua siri'''
 
Lakini ni nini kilichotokea baada ya dola ya Warumi kuvunjika katika karne ya 5 B. K. Haikufuatiwa na dola nyingine yoyote kuu, na kwa kweli haijakuwapo dola ya tano ya kulinganishwa kimamlaka, pamoja na kuwepo jitihada kubwa za watu wenye tamaa kuunda nyingine. Maeneo ya dola ya Kirumi yalimeguka kutokana na uvamizi wa makabila jeuri ya Kihan, Kigoti, Kivisigoti na Kivandali, yaliyoanzisha tawala zao wenyewe tofauti. Mataifa ya sasa ya Ulaya yametokana na falme hizo. Katika kipindi chote cha historia ya miaka 1500 mpaka sasa, mataifa hayo yamebakia katika mgawanyiko, kama ilivyoashiriwa na nyayo za ile sanamu – nusu chuma na nusu udongo: “ nusu una nguvu, na nusu yake umevunjika … hawatashikamana. “(Dan. 2:42-43)
 
Line 201 ⟶ 191:
 
'''NYAKATI TULIZO NAZO'''
 
Ingawa unabii tuliouzingatia mpaka sasa umeendelea kutimia hadi hivi leo, ulihusu zaidi matukio ya siku nyingi za nyuma (ukiacha urudishwaji upya wa Waisraeli hivi karibuni katika ardhi yao ya kale). Je, kuna kinachosemwa na unabii wa Biblia juu ya nyakati tulizo nazo kuweza kutuongoza katika siku hizi?
 
Line 207 ⟶ 196:
 
'''Amani na maendeleo?'''
 
Kinyume cha matazamio hayo, matukio ya karne ya 20 yamekuwa mfadhaiko. Ndoto za maendeleo na amani zimefifia. Vita viwili vibaya sana vya dunia, vikiwa vimechinja mamilioni na kuleta uharibifu usiosemekana wa mali na mateso, vimefuatiwa na uundaji wa silaha kali za maangamizi ambazo hazijawahi kutengenezwa. Mawazo ya utatuzi ya aina mbalimbali ya ‘wenye busara’ wa karne ya 19 yamekuwa bure. Kupanuliwa elimu hakujafuatiwa na maadili zaidi, badala yake na kukua kwa dhuluma, choyo, vurugu na uvunjaji sheria. Dini ya Kikristo, mbali na kuwabadili mataifa, imekuwa katika kurudi nyuma duniani pote.
 
Line 221 ⟶ 209:
 
'''Mashaka na hofu duniani'''
 
Kwa hiyo yale anayoendelea kusema lazima yahusiane na siku hizo – siku za Israeli kurudishwa katika nchi yao wenyewe. Hivi ndivyo anavyotabiri.
 
Line 237 ⟶ 224:
 
'''HITIMISHO'''
 
Kuna majumuisho kadhaa muhimu tunayoweza kuyafikia kutokana na kuchunguza kwetu unabii wa Biblia.
 
Line 259 ⟶ 245:
 
'''Kitu cha muhimu'''
 
Lakini bila shaka kuna zaidi. Unabii huu wa ajabu unapatikana katika Biblia, na sio mahali pengine popote duniani. Hakuna maandiko mengine, hakuna vitabu, hakuna matamko mengine yoyote ya mwanadamu yanayoweza hata kwa mbali kulinganishwa na Biblia. Lakini Biblia inatuambia kwamba Yesu alikuwa mwana wa Mungu; mambo aliyosema yamehifadhiwa kwa ajili yetu katika Injili za Agano Jipya. Pamoja na mafundisho ya mitume wake Petro, Yohana na Paulo, wanatufunulia ukweli ambao hatuwezi vinginevyo kuujua. Wanatuonya juu ya ukweli kuhusu kifo; wanaeleza kwa nini Injili ni ‘habari njema,’ ‘uweza wa Mungu uuletao wokovu’ (Warumi 1:16). Wanatutia moyo na ahadi ya uzima wa milele katika mpango mpya atakaouanzisha Kristo atakapokuja. Ndio maana inatupasa kuisoma Bilia. Inaweza kutupa utofauti wa muhimu kati ya utupu wa kifo, na tumaini la nguvu la maisha yasiyo na mwisho.