Adalbert wa Magdeburg : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
New page: 200px|thumb|Mtakatifu Adalbert wa Magdeburg '''Mtakatifu Adalbert wa Magdeburg''' (alifariki tarehe 20 Juni, 981) alikuwa askofu mkuu wa kwanza...
(Hakuna tofauti)

Pitio la 12:28, 3 Julai 2008

Mtakatifu Adalbert wa Magdeburg (alifariki tarehe 20 Juni, 981) alikuwa askofu mkuu wa kwanza wa mji wa Magdeburg, Ujerumani. Ametambuliwa kuwa mtakatifu. Sikukuu yake ni 20 Juni.

Mtakatifu Adalbert wa Magdeburg

Maisha

Adalbert alizaliwa Ujerumani na kuwa mtawa katika mji wa Trier. Baada ya kuwekwa wakfu kama askofu, mwaka wa 961 alitumwa mjini Kiev, Urusi kama mmisionari. Kundi lake lote liliuawa, naye Adalbert peke yake aliweza kurudi Ujerumani. Baadaye aliteuliwa kuwa askofu mkuu wa dayosisi ya Magdeburg. Alianzisha madayosisi mapya pengi upande wa Mashariki wa Ujerumani, kama katika miji ya Naumburg, Meißen, Merseburg, Brandeburg, Havelberg, na Poznan. Mwanafunzi wake mmoja aliyetakatifishwa kama yeye ni Adalbert wa Praha.

Tazama pia

Viungo vya nje