Kitabu cha Yuditi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
New page: '''Kitabu cha Yudith''' ni kimojawapo kati ya vitabu deuterokanoni vya Biblia. Kimo katika Septuaginta na katika Agano la Kale la Kanisa Katoliki, la Waortodoksi ...
(Hakuna tofauti)

Pitio la 21:04, 24 Julai 2008

Kitabu cha Yudith ni kimojawapo kati ya vitabu deuterokanoni vya Biblia.

Kimo katika Septuaginta na katika Agano la Kale la Kanisa Katoliki, la Waortodoksi wengi na la baadhi ya Waprotestanti, lakini si katika Tanach ya Uyahudi wala katika Biblia ya Waprotestanti.

Hadithi hiyo, iliyoandikwa katika karne ya 1 K.K. inahusu wakati wa mfalme Nebukadneza, na vita vyake dhidi ya Israeli (karne ya 6 K.K.).

Kinyume cha matarajio, Yudith, mwanamke wa kabila la Yuda, aliweza kupata ushindi kwa imani na ushujaa wake.

Habari hiyo ya ajabu ilipata mwangwi kwa wingi katika sanaa mbalimbali.

Wengi wanaona katika Yudith kielelezo cha Bikira Maria katika mapambano dhidi ya shetani.