Kaini : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
New page: Kadiri ya kitabu cha Mwanzo (Biblia) katika Agano la Kale wana wawili wa kwanza wa Adamu na Hawa, majina yao Kaini na Habili, walitunza imani yao kwa Mungu ...
 
No edit summary
Mstari 3:
Tabia na maisha ya watoaji wa sadaka ina maana kuliko vitu wanavyovitoa, kwa hiyo Mungu alimwambia Kaini kuwa, akitaka Mungu ampokee, angepaswa kushinda dhambi iliyokuwa ikitaka kumwangamiza. Dhambi hiyo ilikuwa kama mnyama wa mwitu ajikunjaye na kuotea mlangoni, ili aweze kumshambulia mtu akitoka nje (4:6-7).
 
Kaini hakushinda dhambi yake, na katika [[hasira]] ya [[wivu]]] alimwua Habili. Tendo lake la kutwaa uzima wa ndugu yake lilidai kisasi kwa Mungu aliyetoa uhai ule. Kwa hiyo Mungu alimfukuza Kaini aende mbali na mahali walipoishi watu wengine.
 
Ingawa Kaini alidumu katika hali ya kutotubu, Mungu katika huruma yake kubwa alimlinda asiuawe kwa kisasi (4:8-16).
 
Baadaye [[historia ya wokovu]] inaonyesha kulikuwa na maendeleo ya ufugaji wa kondoo na ng'ombe, pia kulikuwa na maendeleo ya ufundi na [[utamaduni]], lakini kwa upande wa [[maadili]] watu walizidi kuwa waovu.
 
[[Lameki]], licha ya kumwua kijana kwa ajili ya kumwumiza kidogo, alitunga wimbo uliotukuza ukatili wake. Kaini alikuwa afadhali kidogo. Alitafuta na alipata kinga fulani ya Mungu, asije akauawa kwa kisasi, lakini Lameki hakujali jambo lo lote, akatisha sana, mtu asije akathubutu kumdhuru (4:19-24).