Dionysius Exiguus : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
 
No edit summary
Mstari 1:
[[image:scriptorium.jpg|frame|Dionysius Exiguus alianzisha hesabu "[[baada ya Kristo]]"]]
'''Dionysius Exiguus''' (aliishi takriban [[470]] - [[544]]) ni jina la [[mmonaki]] Mkristo aliyeishi mjini [[Roma]] mnamo mwaka 500 BK. Anajulikana zaidi kama mtaalamu aliyeanzisha hesabu ya miaka "[[baada ya Kristo]]".
 
Dionysio alikuwa mwenyeji wa Scythia (Romania ya leo) akawa mmonaki na kuhamia Roma alipoheshimiwa kwa sababu ya elimu yake. Alitafsiri maandiko mengi kutoka lugha ya [[Kigiriki]] mkwa [[Kilatini]].
Mstari 7:
 
==Anno Domini==
Wakati wake ilikuwa jambo gumu kukadiria tarehe za kihistoria. Watu walitumia mahesabu mbalimbali. Wengi waliendelea na desturi ya zamani ya kutaja mwaka wa [[Konsuli wa Roma|"konsuli"]] iliyokuwa cheo kikuu Roma mjini. Lakini makonsuli walibadilika kila mwaka ikawa utaratibu mgumu kwa kazi ya kihistoria. Wakristo wengi walifuata desturi ya [[Misri]] wakihesabu miaka tangu [[Diokletiano]] aliyekumbukwa kwa sababu mateso yake makali dhidi ya Wakristo. Lakini Dionysio hakupenda kukumbuka mtawala aliyedhulumu Wakristo. Hivyo alikadiria mwaka wa kuzaliwa kwake Yesu.
 
Hesabu hii inaitwa "anno Domini" yaani "katika mwaka wa Bwana (Yesu)" (anno= [[kilat.]] "mwaka"; Domini = Kilat. "Bwana"). Kifupi chake ni "AD".
Mstari 14:
 
==Uenezaji wa hesabu ya Dionysio==
Mwanzoni hesabu ya Dionysio haikujulikana isipokuwa kati ya wataalamu wachache. Wafalme wa [[Ulaya]] walipendelea kuhesabu miaka ya utawala wao wakiiga mfano wa Waroma wa Kale.
 
Lakini kanisa katoliki lilianza polepole kutumia hesabu yake. Mnamo mwaka [[1000]] ilikuwa kawaida katika hati rasmi za Ulaya.
 
==Kosa la Hesabu ya Dionysio==
Hesabu ya Dionysio ina kosa la miaka kadhaa. Wakati wake [[Dola la Roma]] lilikuwa limeshakwisha katika Italia, [[Kaisari]] alikaa [[Bizanti]] au [[Roma ya Mashariki]]. Kumbukumbu za Roma yenyewe hazikutunzwa tena tangu miaka mingi. Leo hii wataalamu wengi hukubaliana ya kwamba kasoro la Dionysio ni takriban miaka 4 - 8; yaani mwaka halali wa kuzaliwa kwake Yesu ulikuwa kama miaka nne hadi nane kabla ya mwaka ambao tumezoea kuhesabu kama "1".

Wengi walijaribu kusahihisha kosa hili lakini habari kamili kabisa hazipatikani tena.
 
[[Category:Kalenda]]