Tofauti kati ya marekesbisho "Fonolojia"

1,373 bytes added ,  miaka 12 iliyopita
no edit summary
d (roboti Nyongeza: ky:Фонология)
'''Fonolojia''' ni tawi la sayansi ya [[isimu]]. Inashughulikia uchunguzi wa mfumo wa sauti katika lugha fulani, kwa mfano ugawanyaji wa [[irabu]] na [[konsonanti]]. Matokeo ya uchunguzi wa kifonolojia yana umuhimu katika kubuni [[alfabeti]]. Dhana ya fonolojia inajipambanua vizuri zaidi ikifasiliwa kwa kutofautishwa na fonetiki. Wakati fonetiki ni taaluma inayochunguza sauti zitamkwazo na binadamu bila kuzihusisha na lugha yoyote, fonolojia huchunguza '''mfumo wa sauti wa lugha mahususi kama vile sauti za Kiswahili, Kiingereza, Kimwera, na Kinyaturu. ZINGATIA: Fonetiki huchunguza sauti zote zitamkwazo na binadamu; fonolojia huchunguza MFUMO WA SAUTI wa lugha mahususi.
 
Hivyo, fonetiki huchunguza sauti nyingi kadri iwezekanavyo, lakini fonolojia huchunguza sauti chache tu zilizomo katika mfumo wa sauti wa lugha husika. Mathalani, mfumo wa sauti wa lugha ya Kiswahili una sauti thelathini tu (irabu tano na konsonanti ishirini na tano).
 
Jambo lingine la kuzingatia ni vipashio vya kiuchambuzi vya matawi haya mawili. Wakati fonetiki kipashio chake cha msingi ni FONI, fonolojia kipashio chake cha msingi ni FONIMU. Kwa kuzingatia maelezo ya hapo awali, ni wazi kuwa FONI ni nyingi zaidi kuliko FONIMU, kwakuwa FONI ni kila sauti itamkwayo na binadamu, wakati FONIMU ni sauti zile tu zilizomo katika mfumo wa sauti wa lugha mahususi. Hivyo, kuna FONIMU za Kiswahili, za Kiingereza, za Kichina, n.k., lakini FONI si za lugha yoyote na wala uwezi sema kwa uhakika kuna FONI ngapi, kwakuwa bado kuna lugha nyingi duniani ambazo bado hazijatafitiwa.
 
Mchangiaji: achipila@yahoo.co.uk, 11:22, 19 Sept. 2008.
==Marejeo==
*[[TUKI]] 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", [[Chuo Kikuu cha Dar es Salaam]]
Anonymous user