Tofauti kati ya marekesbisho "Mchezo wa ng'ombe"

106 bytes removed ,  miaka 15 iliyopita
no edit summary
No edit summary
No edit summary
'''Mchezo wa Ng'ombe''' ni desturi inayojulikana hasa katika nchi za [[Hispania]] na [[Ureno]]. Imekuwa pia mila ya pekee kwenye [[Kisiwa cha Pemba]], [[Tanzania]].
 
==Asili za Roma ya Kale==
Historia ya desturi hii inarudi nyuma hadi zamani za [[Dola la Roma]] watu walipopenda kuwa na maonyesho ya mapambano ya wanyama pori, ama ya wenyewe kwa wenyewe au zaidi ya watu dhidi ya wanyama hawa. Maonyesho haya yalifanyika katika uwanja wa mji kwa mfano uwanja wa [[Koloseo]] huko [[Roma]]. Desturi hii imepotea kila sehemu ya eneo la kale la Dola la Roma kwa sababu ilipingwa na kanisa la kikristo isipokuwa [[Hispania]] na [[Ureno]]. Ilhali Wahispania wanaua ngombe wa dume Wareno wanawachezea tu hadi kuwaangusha chini bila kuwaua. Wahispania walipeleka mchezo hadi [[Amerika ya Kusini]] kama vile [[Mexiko]]. Kwa [[Kihispania]] wale wanoshindana uwanjani na ng'ombe dume wanaitwa "torero"; mkuu wao atakayemwua kwa pigo la upanga wake ni "matador".
 
Ilhali Wahispania wanaua ngombe wa dume Wareno wanawachezea tu hadi kuwaangusha chini bila kuwaua. Wahispania walipeleka mchezo hadi [[Amerika ya Kusini]] kama vile [[Mexiko]]. Kwa [[Kihispania]] wale wanoshindana uwanjani na ng'ombe dume wanaitwa "torero"; mkuu wao atakayemwua kwa pigo la upanga wake ni "matador".
 
==Mchezo wa ng'ombe Pemba kisiwani==
 
Kuhusu mchezo huu amesema Abdullah Amur Suleiman (http://groups.msn.com/SitiBintiSaad/mchezowangombebullfight.msnw):
 
''Mchezo wa ng’ombe ni mchezo wa taifa huko Pemba, hapana mtoto wa kiume hata mmoja wa Kipemba, akiwa mwenye asili ya Kiafrika au Kiarabu ambaye hajuwi kumcheza Ng’ombe.
 
''Mchezo huu jinsi unavyopendwa na vijana wa kiume wa Pemba ni kama vile wavulana wanavyoupenda mchezo wa mpira yaani ‘football’, huko Zanzibar, Tanzania bara na kwingineko ulimwenguni.''
 
''Aghlabu mchezo wa ng’ombe huchezwa wakati wa watu ambao wamerejea mavunoni na karafuu zimekwisha tena na hapo hutazamiya kustarehe. Watu wengi hujumuika kwenye sherehe hizo za mchezo wa ng’ombe na hawaji tu kuona mchezo huo lakini hulipa ada maalum kwa ajili ya kuuona namna mchezo huo ufanywavyo na mastadi wake hodari.''