Khalifa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
 
No edit summary
Mstari 1:
[[Image:Califate 750.jpg|thumb|350px|Eneo la utawala wa makhalifa wakati wa mwisho wa Wamuawiya mw. 750]]
'''Khalifa''' ni cheo cha kihistoria kwa ajili ya kiongozi wa ''[[ummah]]'' (jumuiya ya [[Uislamu]]). Ni neno la Kiarabu <big><big> خليفة </big></big>''khalīfah'' linalomaanisha "makamu". Khalifa ni kifupi chake cha<big><big> خليفة رسول الله </big></big> "khalifat-ur-rasul-Allah" kinachomaanisha "Makamu wa mtume wa Allah/Mungu". Hivyo mana yake ni makamu au mfuasi wa [[Mtume Muhammad]] katika nafasi yake kama kiongozi wa Waislamu.
 
Line 15 ⟶ 16:
 
==Wamuawiya, Waabbasi na Waosmani==
===Wamuawiya===
Wafuasi wa Muawiya waliendelea kutawala hadi [[750]] walipopinduliwa na wafuasi wa Abbas mjomba wa mume Muhammad. Mmuawiya mmoja tu aliweza kukimbia hadi sehemu ya [[Hispania]] iliyotekwa na Waarabu alipopokelewa kwa heshima na kuanzisha Ukhalifa wa Wamuawiya wa [[Cordoba]] uliodumu katika Hispania hadi [[1031]].
===Waabbasi===
Waabbasi walitwala mjini [[Baghdad]] hadi mnamo mwaka [[945]]. Baadaye nguvu ya kitawala ilikuwa mkononi wa viongozi wa vikosi vya ulinzi wasiokuwa Waarabu lakini Wajemi au Waturuki. Mwaka [[1258]] [[Wamongolia]] walishambulia na kuharibu mji wa Baghdad na kumwua khalifa [[Al-Mustasim]]. Mjomba wake [[al-Mustansir]] aliweza kukimbilia [[Misri]] alipopewa cheo cha Khalifa na mtawala wa nchi Sultani [[Baibars]]. Makhalifa waliomfuata katika Misri walikuwa viongozi kwa jina tu waliowategemea kabisa watwala wa Misri.
 
Mwaka [[1517]] khalifa wa mwisho wa Waabbasi [[Al-Mutawakkil III]] alikamatwa na Waturuki [[Waosmani]] walipovamia Misri. Wakampeleka [[Istanbul]] kama mfungwa alipokabidhi cheo chake pamoja na simi na koti ya Mtume Mohammad kwa [[Sultani Selim I]].
 
===Waosmani===
Watawala Waosmani hawakujali sana cheo cha khalifa. Walijiita hasa "Sultani" pamoja na vyeo vingine. Walitumia cheo cha khalifa hasa katika uhusiano na Waislamu nje ya dola lao. Kwa mafano wakishambulia nchi za Kiislamu kama Uajemi walijiita Khalifa wakidai utii kama wakuu wa Waislamu wote. Au wakishambuliwa na [[Austria]] au [[Urusi]] walitumia cheo cha khalifa kuita Waislamu wote kujiunga na [[jihad]] ya kivita.
 
Safari ya mwisho ya kutumia cheo cha khalifa kwa wito la jihad ya kivita ilitokea wakati wa [[Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia]] ambako Sultani [[Mehmed V]] alitumia tena cheo chake cha khalifa kuita waislamu wote wa dunia kujiunga na vita dhidi ya [[Uingereza]].
 
===Mwisho wa ukhalifa===
Baada ya vita cheo kilifutwa na bunge la Uturuki kwa mapendekezo ya [[Atatürk]] mwaka [[1924]].
 
===Khalifa mbalimbali wa kihistoria===
Nje ya ufuatano rasmi ya makhalifa kulitokea pia cheo cha khalifa katika maeneo mbalimbali kwa kushhindana na khalifa rasmi ni nani mwenye cheo cha kweli.
 
Mifano ni:
* Makhalifa [[Wafatima]] (wa Shia) katika Misri na Afrka ya Kaskazini (909-1171).
* Makhalifa wa [[Muwahidun]] katika Afrika ya Kaskazini na Hispania ya Kiislamu (1145-1269).
* Makhalifa wa [[Ahmadiyya]] - waliomfuata Hazrat [[Mirza Ghulam Ahmad]] kama kiongozi wa Ahmadiyya huitwa "khalifa". Tangu 22 Aprili [[2003]] Hazrat Mirza Masroor Ahmad amekuwa "khalifatul masih V) (khalifa wa tano wa Messia).
* makhalifa wa [[Sudan]]: wafuasi wa Al-Mahdi waliitwa kwa cheo "khalifa".
 
 
==Majaribio ya kukufusha ukhalifa==
Tangu mwaka huu walijitokeza viongozi wa vikundi mbalimbali waliodai cheo cha khalifa lakini bila kukubaliwa na Waislamu wengi. Mfano mmojawapo ni kundi la Mturuki Cemaleddin Kaplan alijejitangaza 1994 kuwa khalifa. Alikuwa na wafuasi maelfu kadhaa kati ya Waturuki katika Ujerumani. Baada kifo chake mashindano juu ya cheo kilisababisha kuuawa kwa mfuasi mmoja na kikundi kilipigwa marufu na serikali ya Ujerumani.
 
Kati ya wafuasi wa Uislamu wenye mwelekeo mkali kuna mafundisho ya kwamba cheo cha khalifa kinapaswa kurudishwa kama utaratibu wa kisiasa cha kufaa.