Waamuzi (Biblia) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: an:Libro d'os Chuezes
No edit summary
Mstari 1:
Kitabu cha [[Waamuzi]] ni cha saba katika orodha ya [[Biblia ya Kiebrania]] na kinaletaya [[Agano la Kale]] la [[Ukristo]].

Kinaleta mapokeo mbalimbali kuhusu historia ya [[Israeli]] kwenye miaka 1200-1025 hivi [[K.K.]]
 
Kama vitabu vingine vyote vya [[Biblia]], hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa [[Historia ya Wokovu|historia ya wokovu]] ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya [[Ufunuo|ufunuo]] wa [[Mungu]] kwa [[binadamu]].
 
Baada ya [[makabila 12 ya Waisraeli]] kugawana nchi takatifu, kila moja likaanza kujitegemea: lakini bila ya umoja hakuna nguvu upande wa dini wala wa siasa.
Line 13 ⟶ 17:
Mmojawao ni [[Gideoni]] aliyedumisha amani kwa miaka 40. Alipoitwa na Mungu alijitetea kwa kusisitiza udogo na ufukara wake, lakini akajaliwa ishara zote alizoziomba ili kuhakikishiwa msaada (Amu 6:11-24,36-40). Sura ya 7 inasimulia Mungu alivyopunguza askari wake ili ionekane wazi kuwa ushindi ni wa Mungu mwenyewe, hautegemei uhodari na wingi wa watu au silaha zao. Ni kawaida ya kazi ya Mungu kuonyesha uweza wake katika udhaifu wa binadamu. Waisraeli walipotaka Gideoni awe mfalme wao, akakataa katakata ili Bwana tu aendelee kuwatawala (Amu 8:22-23), lakini wazo hilo likaendelea kuenea, ingawa wengine walilipinga (Amu 9:1-21).
 
==Mazingira==
'''MAZINGIRA'''
 
Kitabu cha Waamuzi kinashughulika na matukio ya Israeli wakati wa miaka mia mbili hivi baada Yoshua kuiteka nchi ya Kanaani. Chini ya Yoshua Waisraeli walishinda vita vile vikubwa, lakini watu hawakutii amri ya Mungu ya kuwaangamiza Wakanaani wote. Matokeo yake, Wakanaani waliobaki nchini kila wakati walisababisha matatizo katika Israeli, kwa upande wa dini na kwa upande wa siasa pia.
Line 21 ⟶ 25:
Watu wale walioleta wokovu waliitwa Waamuzi, kwa sababu walitimiza uamuzi wa Mungu, wakiwashinda maadui na kuwaokoa watu wake. Wengine wasiokuwa watu wa vita, walitimiza uamuzi wa Mungu kwa njia ya kuongoza mambo ya kila siku ya watu wa Mungu kadiri ya sheria yake. Kutokana na viongozi wale, wakiwa wa kiraia au wa kijeshi, kitabu hiki kilipata jina lake.
 
'''==Waisraeli na maadui zao'''wao==
 
Inaonekana kwamba vita mabalimbali vya mataifa ya jirani na ushindi wake, na mapinduzi ya baadaye yaliyoletwa na Waamuzi wa Israeli, mara nyingi zaidi yalikuwa katika sehemu fulani ya nchi tu, bila ya kuingia katika nchi yote ya Kanaani. Kwa kawaida makabila yaliyohusika yalikuwa yale ya maeneo yao tu. Pia iliwezekana kwamba ushindi na mashambulio yake yalikuwa sehemu mbalimbali kwa wakati mmoja. Kwa mfano, habari za Yefta na Waamoni ziliweza kuwa zimetokea wakati ule ule ambao Samsoni alishughulika na Wafilisti (taz. 10:7-8; 11:5; 13:1). Haukuwepo umoja sana katika Israeli, na kila kabila, au hata makundi ya makabila fulani, yaliangalia mambo yaliyotokea katika maeneo yao, bila kujali mambo ya makabila mengine.
Line 29 ⟶ 33:
Matengano yale ya makabila ya Israeli hayakuwa ya kisiasa au ya kieneo tu, bali pia yalileta shida kwa umoja wa kidini, kwa sababu watu wengi walitengwa na mahali maalumu pa kuabudia, yaani hema la kukutania lililokuwepo Shilo (Yos 18:1; 22:9). Kwa kifupi, matatizo yote ya Waisraeli, yakiwa ya maendeleo, ya kisiasa au ya kidini, yalitokana na ukosefu wa watu wa kutii amri ya Mungu ya kuwaangamiza Wakanaani kabisa (taz.1:21, 27-36; Kum 7:2-4; 9:5; Yos 24:14-24).
 
'''==Dini za Wakanaani'''==
 
Miungu ya Wakanaani ilijulikana kwa jina la Baalim au Mabaali (wingi wa Baali; taz. 2:11; 10:10; 1 Fal 16:31), na miungu ya kike iliitwa Maashtorethi (wingi wa Ashtorethi; taz. 2:13; 1 Sam 7:3-4), na Asherimu au Ashera (wingi wa Ashera; taz. 6:25-26; 2 Fal 23:4; kumbuka pia 'Uasherati'). Miungu ile ilikuwa ya kustawisha uzazi wo wote, pia iliaminiwa kuwa ingeweza kuongeza ustawi wa mimea. Waisraeli walijua kwamba Mungu alikuwa Mwumbaji wa hali yote ya uzazi na ustawi, na hivyo ilikuwa hatua ndogo tu kwa Waisraeli kuunganisha na kuchanganya mawazo ya Kikanaani na ujuzi wao wenyewe, na hivyo kumwabudu Yahweh kama Baali mwingine. Maana ya neno 'baali' ilikuwa bwana, mume, au mwenyewe. Waisraeli walimjua Yahweh (Yehova) kuwa Mume na Bwana wao, kwa hiyo walikuwa katika hatari zaidi ya kuunganisha Mabaali wa Kikanaani na Mungu wao aliye Yahweh (Hos 2:5-10).
Line 37 ⟶ 41:
Makahaba wa kike na wa kiume walipatikana katika 'mahali pa juu' kwa ajili ya sherehe mbalimbali za uzazi na ustawi wa nchi. Sherehe zile zilikuwa za kidini nao waliamini kwamba sherehe hizo za kuingiliana kimwili zingestawisha nafaka, mifugo yo yote na hata maisha ya kifamilia (1 Fal 14:23-24; Yer 13:27). Katika kuyafuata mambo ya Mabaali, watu wa Israeli walikuwa na hatia ya zinaa ya kidini pia. Agano baina ya Waisraeli na Mungu lilifananishwa na kufungwa ndoa, na hivyo Waisraeli walipojiunga na Mabaali na miungu mingine, walifanya dhambi ya zinaa (taz. 2:12-13, 17; Yer 2:20; 3:6-8; Hos 2:13; 4:12).
 
==Yaliyomo==
'''YALIYOMO'''
 
1:1-2:10 Muhtasari wa ushindi wa Yoshua
Line 48 ⟶ 52:
* [http://www.cbm-tz.org/swahili/commentary/commentary.htm CBM Biblia Inasema]
 
{{Biblia AK}}
[[Category:Dini]]
 
[[Category:Vitabu vya Agano la Kale]]
[[Category:Watu wa Biblia]]