Jalidi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
New page: thumb|right|225px|Majani yaliyofunikwa jalidi '''Jalidi''' ni hali ya baridi ambako halijoto inafikia chini ya kiwango cha sentigredi 0. Hii ni kiwango ambako ...
(Hakuna tofauti)

Pitio la 11:13, 8 Novemba 2008

Jalidi ni hali ya baridi ambako halijoto inafikia chini ya kiwango cha sentigredi 0. Hii ni kiwango ambako maji yanaanza kuganda kuwa barafu. Hivyo "jalidi" ni pia jina la umande ulioganda kutokana na baridi kali ukionekana kama theluji.

Majani yaliyofunikwa jalidi

Jalidi kama halijoto inaathiri viumbehai na mimea kwa sababu huwa na maji katika miili yao. Mimea inakufa katika hali ya jalidi kama maji ndani ya seli zao inaganda; maji ikiganda inapanua mjao wake hivyo kupasua seli.

Mimea ya nchi ambako jalidi ni hali ya kawaida wakati wa majira ya baridi ina uwezo wa kukauka kabla ya majira ya jalidi kuanza. Katika mazingira ya joto mimea hufa mara nyingi kama baridi huwa kali.