Tofauti kati ya marekesbisho "Waraka kwa Wakolosai"

271 bytes added ,  miaka 11 iliyopita
no edit summary
d (roboti Nyongeza: tl:Sulat sa mga taga-Colosas)
 
Barua kwa [[Wakolosai]] ni kati ya vitabu 27 vya [[Agano Jipya]] ambalo pamoja na [[Agano la Kale]] linaunda [[Biblia]] ya [[Wakristo]].
 
Kama vitabu vingine vyote vya [[Biblia]], hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa [[Historia ya Wokovu|historia ya wokovu]] ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya [[Ufunuo|ufunuo]] wa [[Mungu]] kwa [[binadamu]].
 
==Muda wa uandishi==
 
Barua hiyo ni mojawapo kati ya zile za mwishomwisho za [[Mtume Paulo]] na inaonyesha maendeleo ya [[teolojia]] yake, hasa kutokana na muda mrefu wa kutafakari aliojaliwa kifungoni.
 
==Mazingira==
 
[[Kanisa]] la [[Kolosai]], mji wa biashara karibu na [[Efeso]] lilianzishwa na mwanafunzi wa Paulo, labda [[Epafra]], halafu likaingiwa na mafundisho ya ajabuajabu yaliyochanganya mambo ya [[Kiyahudi]] na ya Kipagani na yaliyozingatia mno ukuu wa [[malaika]] juu ya ulimwengu.
 
Hakuna sababu ya kutafuta kwingine [[hekima]] na maarifa, wala ya kujiwekea masharti ya kibinadamu yasiyosaidia kuokoka (Kol 1:13-29; 2:6-3:4; 3:5-17).
 
==Mpangilio==
 
Mpangilio wa barua ni kama kawaida ya barua za Paulo: utangulizi, mafundisho ya imani, maonyo kuhusu uzushi, mawaidha na hatima.