Tendo la ndoa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
+jamii; +en; {{fupi}} - yaani ina sentensi moja tu
No edit summary
Mstari 1:
'''Tendo la ndoa''' ni kitendo cha kujamiiana kati ya mwanamke na mwanaume.
 
===Mkamilishano===
 
[[Jinsia]] zinalenga kukamilishana katika [[ndoa]]. Kadiri ya [[Biblia]] [[Mungu]] baada ya kumuumba [[Adamu]] alisema, “Si vema mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye” (Mwa 2:18).
 
Umbile la [[mwanamume]] linaelekea kukamilishana na lile la [[mwanamke]] kiroho na kimwili. Lakini [[roho]] haionekani, hivyo ni rahisi zaidi kuona jinsi miili yao inavyofaa kuungana iwe [[mwili]] mmoja.
 
Hata hivyo tuelewe mkamilishano huo unafanyika katika [[nafsi]] pia, ambazo zina [[vipawa]] tofauti vinavyowezesha kwa pamoja kukabili vizuri [[maisha]] ya nyumbani, ya [[uchumi]], ya [[siasa]], ya [[dini]] n.k.
 
===Uzazi===
 
Tukiangalia [[viungo vya uzazi]] vya kike tunakuta kwenye kilango chake [[kizinda]], yaani [[nyama]] nyembamba inayoondolewa na mwanamume wa kwanza anayekiingilia. Ndiyo sababu ni kama mhuri wa [[ubikira]] wa mwanamke. Katikati ya kizinda kuna tundu dogo tu kupitishia [[damu]] wakati wa [[hedhi]], yaani siku zile ambazo anatokwa damu kupitia [[uke]] ulio nafasi ya wazi (kati ya kizinda na [[tumbo la uzazi]]) iliyo tayari kupokea [[uume]] na [[mbegu]] zake.
 
Hizo zinasafiri muda wa saa sita hivi katika tumbo la uzazi ili kukifikia [[kijiyai]] katika [[mrija]] unaoliunganisha na [[kifuko cha kijiyai]]. Mbegu zinazofunga safari hiyo zinaweza kuwa milioni kadhaa, lakini chache tu zitafika; tena kati yake, moja tu itapenya kijiyai, kwa sababu mara tu inapoingia kijiyaji kinakuwa kigumu kwa nje, hivi kwamba mbegu nyingine zitagonga bure. Ikiwa mbegu hiyo inabeba [[kromosomu Y]] [[mtoto]] atakuwa wa kiume, la sivyo atakuwa wa kike.
 
Mbegu na kijiyai vinapounganika, [[viini vya urithi]] vinavyobebwa navyo vinachanganyikana kwa namna mojawapo kati ya zile zote zinazowezekana. Kwa kawaida viini hivyo ni 46 kwa kila [[binadamu]], na kila [[seli]] ya mwili wake inavyo. Katika viini hivyo zimo [[jeni]] 25,000 hivi, yaani sifa zote za mtu huyo maalumu tangu atungwe hadi afe.
 
Viini hivyo vinaongoza ujenzi wa mwili kwanza tumboni mwa mama, halafu utengenezaji wa seli mpya baada ya kuzaliwa. Hata mbegu zote zina viini hivyo vya [[baba]], na vijiyai vyote vina viini hivyo vya [[mama]], isipokuwa katika kukomaa vinapungua na kubaki 23 tu kusudi mbegu na kijiyai vikiungana [[mimba]] inayopatikana iwe na viini 46 kama kawaida.
 
Kutokana na wingi usiohesabika wa namna ambazo jeni hizo zinaweza kuchanganyikana, hakuna mtu aliye sawa na mwingine, kama vile [[alama za vidole]] zilivyo tofautitofauti. Hivyo toka mwanzo mimba hiyo ni mtu wa pekee, ingawa ina seli moja tu. Seli hiyo itakua na kuanza kugawanyika katika seli 2, 4, 8, 16 n.k.
 
Ingawa kila moja ina viini vilevile, polepole seli zinatofautiana ili kufanya kazi maalumu ([[ubongo]], [[moyo]] na [[viungo]] vingine) na kushirikiana zote vizuri katika umoja wa mwili. Baada ya miezi miwili viungo vyote vimeshatengenezwa, halafu vinazidi kukua na kukamilika hadi mwezi wa tisa ambapo mwishoni mwake mtoto atazaliwa.
 
{{mbegu}}
 
{{fupi}}
 
[[Category:Jamii]]
[[Category:Biolojia]]
 
[[en:Sexual intercourse]]